DC KIGOMA AWATAKA WANANCHI KULINDA MAZINGIRA KWA KUTUMIA NISHATI SAFI
FROLENCE MASUNGA MWAKILISHI ENVOTEC Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Mohamed Chuachua, ametoa wito kwa wananchi wilayani humo kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan, kwenye ajenda ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kulinda na kuhifadhi mazingira. Rashid Chuchua Dc Kigoma Dkt. Chuachua ametoa wito huo wakati wa akizindua ugawaji wa majiko sanifu ya kupikia ya gharama nafuu yenye ruzuku ya serikali, kwa wananchi katika kata ya Simbo wilayani Kigoma, ambapo amesema kuwa matumizi ya majiko sanifu ni hatua muhimu ya kubana matumizi na zaidi kulinda na kuhifadhi mazingira, kwa kuwa majiko hayo yanatumia nishati kidogo. Kampuni ya ENVOTEC iliyopewa dhamana ya kuuza majiko hayo kwa bei ya ruzuku kupitia Wakala wa Nishati Vijijini REA, kwa ujumla imegawa majiko 1,404 kwa wilaya ya Kigoma, ambapo mwakilishi wa kampuni hiyo Florence Masunga, amesema wananchi watachangia asilimia 15% tu ya bei huku serikali ikilipia asilimia 85%. . Baadhi ya wananchi waliopata majiko...