WATUMISHI SITA IDARA YA AFYA MKOANI KIGOMA WAMEKUFA MAJI ZIWA TANGANYIKA
Watu sita ambao ni watumishi wa idara ya afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wamethibtika kufa, watatu wakiwa bado hawajapatikana wengine tisa wakiokolewa wakiwa hai baada ya boti waliokuwa wanasafiria kuzama katika Ziwa Tanganyika katika Kijiji cha Kalalangabo wilayani humo.
Akithibitisha vifo hivyo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon
Sirro, amesema tukio hilo limetokea mapema leo Ijumaa Machi 13, 2026 asubuhi,
wakati watumishi hao wakisafiri kwenda kijiji cha Kagunga kwa ajili ya kutoa
chanjo kabla ya boti yao kupigwa na dhoruba kufuatia upepo mkali na kupinduka.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kigoma,
Mrakibu Msaidizi Michael Maganga, amesema zoezi la kuwatafuta watu watatu watumishi
wa idara ya afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, miongoni mwa waliopinduka
na boti katika Ziwa Tanganyika eneo la Kalalangabo bado linaendelea.
![]() |
| MichaelMaganga Kaimu Kamanda Zimamoto Mkoa wa Kigoma |
![]() |
| Barozi Simon Sirro Mkuu wa Mkoa wa Kigoma |





Maoni
Chapisha Maoni