Magu yapunguza vifo vitokanavyo na uzazi asilimia 70 kwa miaka mitano

 








Mwanza. Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza imefanikiwa kupunguza Vifo vitokanavyo na uzazi  kutoka vifo 112 hadi 42 katika kipindi cha miaka mitano baada ya serikali kuboresha huduma kwa kutoa vifaa na kuongeza miundombinu ya majengo










Voronica Gibson Mkazi wa Magu

Hellen Chizere Muuguzi mfawidhi Hospitali ya Wilaya ya Magu

Raphaem Mhana Mganga Mkuu W ya Magu

Raphael Mhana Mganga Mkuu Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza ameeleza kipindi cha2015hadi 2020,  hali ilikuwa hairidhishi ikilinganishwa na takwimu kuanzia 2020 hadi 2025  baada ya kufanyika  maboresho katika sekta ya Afya

Hata hivyo Mhana amesema kutokana na maboresho hayo kwa sasa wanatengeza na Miguu bandia ambayo inasaidia Watu wanaopata matatizo mbalimbali zikiwemo ajali

‘’Wagonjwa wenye Matatizo ya Viungo hasa Miguu walemavu wa kuzaliwa na wanaokuwa wamepata ajali katika Wilaya ya Magu na maeneo ya jirani,wamekuwa wakisafiri kwenda mbali kutafuta huduma ya Miguu bandia lakini kwa hivi sasa  baada ya Miguu bandia kuanza kutengenezwa hapa,usumbufu umepungu katika jamii zetu’’amesema Mhana Mganga Mkuu Wilaya ya Magu

 

Kwa upande wake muuguzi mfawidhi wa hospitali ya Wilaya hiyo , Hellen Chizere amesema awali hospitali ilikuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 133 lakini kwa sasa  wanalaza Wagonjwa 176 huku baadhi ya wanawake waliopata pata huduma hospitalini hapo ambao ni Veronika Gibson na Anna Johakimu wakazi wa Magu, wakieleza kuridhishwa na huduma

 

‘’Mimi nilipokuwa nahitaji kujifungua nakufikishwa katika Hospitali ya Wilaya nilihudumiwa Vizuri kwakuandaliwa na wauguzi na Madaktari nikafanyiwa upasuaji nikiwa salma mimi na mwanangu, lakini kilichonivutia ni vifaa ambavyo havikuwepo hapo nyuma maana hii ni mara ya tatu kujifungua katika hospitali hii, maana huduma zinazopatikana kutokana na nyenzo zinatia moyooamebainisha Anna Johakimu mmoja wa wanawake waliokuwa wamepata huduma Hopitali ya wilaya ya Magu

 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

40 CHADEMA KIBONDO WAJIONDOA

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu