Risasi za SMG 599 zafukuliwa ardhini Kibondo
Baadhi ya wakazi wa mji wa Kibondo mkoani Kigoma jana waliingia katika hali ya tahaluki baada ya mafundi ujenzi waliokuwa wakichimba msingi kwa maandalizi ya kujenga nyumba kufukua Lisasi za Bunduki aina ya SMG zipatazo 599 zinazoonekana kukaa muda mrefu ardhini. Mmoja wa wakazi hao Bw, Jastin Samson alisema kuwa kama lisasi hizo zingeweza kuingizwa mitaani kwa kutumiwa na waalifu, kulikuwa na uwezekano wa kuumiza watu wengi Lemijiusi Rabson ambaye alikuwa kibarua katika eneo la ujenzi lililoko katika mTaa wa Ihulilo Kata ya Kibondo mjini Wilayani hapa, amesema kuwa alipokuwa akiendelea na shuguli zake za kuchimba msingi kwa ajili ya maeendalizi ya ujenzi alifukua mkuko wa Sandalusi uliokuwa umewekwa Lisasi ndani yake na kutaarifu kwa msimamizi wake aliyetoe na kuwaita Polisi Msimamizi wa ujenzi huo, Bw, Jackson Amoni aliweka wazi kuwa eneo hilo nila mtu mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Ally mkazi wa kibondo , Mweneyekiti wa Mtaa wa Ihulilo Nu...