sera ya Taifa ya Wazee, haitekelezeki sababu haina sheria
Wazee wa umri wanatambuliwa kuwa ni moja raslimali na nguvu mpya katika maendeleo ya nchi hvyo wanatakiwa kupata fursa za kushiriki katika shuguli za maendeleo sambamba na wananchi wengine
Kulingana na hali ilivyo hivi sasa kwa sababu ya kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili wazee katika jamii umewaathiri wazee walio wengi na kusababisha kukosa huduma mbalimbali stahiki hali inayopelekea kupoteza umuhimu wao
Serikali ya tanzania ilifanya maamuzi ya kuwa na sera ya Taifa ya Wazee mwaka 1999 ambayo ilitungwa mwaka 2003 kwa dhamira ya kuwasaidia kuondokana na changamoto mbambali hatua ambayo imeokana kukwama katika utekelezaji wake kama wanavyoongea katibu mtendaji Bi Clotrida Kokupima mwishoni mwa wiki iliyopita katika kikao kilichoandaliwa na chama cha wazee wilaya ya kasulu mkoani kigoma kwa kuwashirikisha waandishi wa habari
Bi Kokupima alieleza kuwa pamoja na mipango mingi ilimo ndani ya sera hiyo bado wazee wameendelea koukosa huduma kwasababu ya kukosekana kwasheria ya kuisimamia ser hiyo
Chama cha Wazee tawi la Kaslu kimeamua kuitisha kikao hicho na waandishi wa habari ili kujadili vikwazo vinavyowakabili na kuuhabarisha umma ijilikane kinachoendelea na kujenga weredi alisema mwenyekiti wa chama hicho Bw Chubwa Chubwa
Hata hivyo kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Kasulu Bi Elina Kimaro amesema kuwa kwa kutambua hali hiyo waliamua kuweka dirisha kwa ajili ya kutoa huduma kwa Wazee japo yapo matatizo mengi yanayoikabili sekta ya Afya hasa kwa upande wa upatikanaji wa madawa
Kwa kuwa kikao hicho kiliwahusu waandishi wa habari na wazee hao, nao walilazimika kueleza ni namna gani wanavyofanyakazi juu ya maswala yanayowahusu wazee ambapo Dotto Elias toka Tbc 1 na Muhingo Mwemezi wa Clouds Tv
Bi Clotrida Kokupima Katibu Mtendaji Swata Kasulu |
Dotto Elias Tc Kigoma |
Muhingo Mwemezi Clouds Tv Kigoma |
Maoni
Chapisha Maoni