57 Bilion zalipa kaya maskini tasasf mpango wa kunusuru kaya hizo awamu ya kwanza

Washiriki washa ya Tasaf katika Picha ya pamoja  
Omary Malilo kaimu mkurugenzi Tasaf Taifa
Add caption
Toba Mhina Mshiriki
Washiriki wa Warsha Tasaf


Miaka mingi iliyopita Tanzania  lmeendelea kuhesabika kuwa moja ya Taifa masikini  Ulimwenguni,ambapo takwimu za wataalam wa uchumi zinaonaonyesha kukua kwa uchumi wakati watanzania wengi wakiendeleakuishi katika kiwango cha chini cha maisha na dhiki kubwa

Uchumi wa nchi hii unaonekana kukua kwa silimia 6-7%  huku umasikini ukiondoka kwa silimia 2 kutoka kwa wananchi ambao wengi wao utegemea kilimo kuendesha maisha ikiwa nacho  kinakuwa kwa shida kwa silimia 3 tu na kuwaajili watanzania  80% hali inayowanfanya wananchi kuishi kimasikini zaidi

Kutokana  hali hiyo serikali kupitia shirika la mfuko wa maendeleo ya jamii hapa nchini imemue kuweka mpango wake wa kunusuru wananchi wanaoishi katika kaya masikini katika Tasaf awamu ya tatu mango wa kunsuru kaya masikini awamu ya pili kwa kutumia shilingi bilion 57  kama alivyoeleza  Omary Malilo  Kaimu mkurugenzi wa Tasaf makao makuu wakati wa ufunguzi wa semina elekezi iliyoanza jana mjini Kibondo Mkoani Kigoma

Malilo, alisema kuwa hadi kufikia mwezi may mwaka huu shiling bilion 57 zilitumika kuwalipa wanakaya maskini hali ambayo  hadi visasa yapo mabadiriko kwa kiasi fran, na sasa wako katika semina ya kuwaelekeza wataalam wa kada mbalimbali kutoka halmashauri za wilaya juu ya mpango wa kutoa ajira ndogo ndogo katika kaya hizo zilizo kwisha tambuliwa kama anavyoeleza Bw Skalion Luhula mwezeshaji  kitaifa
Nae Bi Doris Gama ambaye pia mwezeshaji katika semina hiyo ameeleza mpango huo jinsi ulivyo kuwa ni kwa ajili ya watu waliokwishatambuliwa na kuingizwa katika mpango ndiyo watakaoshiriki katika awamu ya pili ya kupata ajira ndogondogo katika miradi inayobuniwa na jamii hususa maeneo ya vijijini

Toba Mhina  ni mshiriki wa warsha hiyo ambaye anasema kuwa katika maeneo vijijini zipo changamoto nyingi zinazowakabili wananchi na iwapo mpango huo utakamilika utaleta unafuu katika maenedeleo katika kupata huduma wanazohitaji

‘’Kama katika wilaya ya Uvinza wakati wa kutoa luzuku ya fedha katika malipo juu ya mpango kusuru kaya masiki kwenye utarati wa masharti, maenedeleo yameanza kuonekana kama kupeleka watoto clinic, na Hivi sasa wanafunzi wanajaa mashuleni hadi wanakosa madawati ya kukalia alisema Mhina’’  

Kwa upande wake  Joyce Chuma makam mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo aliwataka washiriki wakati wa utekelezaji wa kazi husika, kujali mazingira kwa kuangalia matumizi ya ardhi Mistu na vyanzo vya maji kwani ni mahitaji muhimu katika maisha ya Binadamu
Mwisho


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji