Risasi za SMG 599 zafukuliwa ardhini Kibondo
Baadhi
ya wakazi wa mji wa Kibondo mkoani Kigoma jana waliingia katika hali ya
tahaluki baada ya mafundi ujenzi waliokuwa wakichimba msingi kwa maandalizi ya
kujenga nyumba kufukua Lisasi za Bunduki aina ya SMG zipatazo 599 zinazoonekana
kukaa muda mrefu ardhini.
Mmoja wa
wakazi hao Bw, Jastin Samson alisema kuwa kama lisasi hizo zingeweza kuingizwa
mitaani kwa kutumiwa na waalifu, kulikuwa na uwezekano wa kuumiza watu wengi
Lemijiusi Rabson ambaye alikuwa kibarua katika
eneo la ujenzi lililoko katika mTaa wa Ihulilo Kata ya Kibondo mjini Wilayani
hapa, amesema kuwa alipokuwa akiendelea na shuguli zake za kuchimba msingi kwa
ajili ya maeendalizi ya ujenzi alifukua mkuko wa Sandalusi uliokuwa umewekwa Lisasi ndani yake na
kutaarifu kwa msimamizi wake aliyetoe na kuwaita Polisi
Msimamizi wa
ujenzi huo, Bw, Jackson Amoni aliweka wazi kuwa eneo hilo nila mtu mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina moja la Ally mkazi wa kibondo ,
Mweneyekiti
wa Mtaa wa Ihulilo Nuhu Kasigwa ameeleza kuwa Eneo hilo lililokuwa likijengwa
nyumba limekaa kwa muda mrefu sana bila kuwepo nyumba na kueleza kuwa kama
hazikuwekwa na watanzania, uenda ziliwekwa na katika ujio wa Wakimbizi toka
nchni Burundi kwani eneo hilo liko karibu maali walipokuwa wakipitia wakimbizi
Aidha Kasigwa amewapongeza vijana hao waliokota
lisasi hizo na kuamua kutoa taarifa Polisi ili taratibu husika zifuate maana
kama wasinge kuwa wenye maadili mema wangeamua kukaa kimya na baadae zikatumika
kuleta madhala katika jamii
Kijana Lemijiusi aliyefukua Rilsasi wakati akichimba msingi |
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni