G7 yatishia kuiongezea Urusi vikwazo

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa, viongozi wa mataifa saba yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi Duniani-G7, wamekubaliana kuwa vikwazo dhidi ya Urusi vinafaa kuendelea.

Bi Merkel amesema hadi pale muafaka wa kukomesha mapigano nchini Ukraine utakapoheshimiwa vikwazo sharti ziendelee.

Akiongea katika siku ya mwisho ya mkutano wa siku mbili, Merkel amesema kuwa mataifa ya G7 yalikuwa tayari kuzidishia Urusi vikwazo zaidi, iwapo hali ingeruhusu.

Kuhusu mzozo wa kifedha unaokumba Ugiriki, Bi Merkel, alionya kuwa muda uliosalia kabla makubaliano hayajatiwa sahihi ni mchache mno.

Alishauri Ugiriki kuchukua hatua madhubuti ilikunusuru sarafu ya taifa hilo.
Viongozi hao wanafanya mazungumzo katika siku ya pili ya mkutano mkuu, wenye nia ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, huku pia swala la kuongezeka kwa makundi yenye itikadi kali likijadiliwa.

Bi Merkel pia amewataka wanachama wa G7 kuchangia hazina ya kuyasaidia mataifa maskini ambayo yanaathirika na mabadiliko ya hali ya anga.

Viongozi kutoka Nigeria na Tunisia watahudhuria kikao maalum, kuhusiana na hatari iletwayo na makundi yenye itikadi kali hasa yale ya Afrika.

Kwa mara ya pili tangu mzozo huo na Ukrain utokee rais Putin wa Urusi hakualikwa kwenye kikao hicho licha ya Urusi kuwa mwanachama wa G7.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji