Vijana raslimali muhimu katika nchi yoyote Duniani hivyo itumike vizuri
Vijana ni
raslimali ya muhimu katika jamii na nchi yoyote Duniani hali inayowataka
kujitambua kuwa wao ni watu wanaotegemewa kama nguvu nguvukazi Taifa hasa hapa
Tanzania
Hayo yaliwekwa wazi na Mwenyekiti wa uhamasishaji
chama cha Mapinduzi wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma Bw, Noberth Bulinjie wakati
wa uchaguzi nafasi wa mbalimbali za umoja wa vijana wa Ccm [Uvccm] uliofanyika
katika ukumbi wa Boma wilayani humo
Bulinjie
aliwataka vijana kujitabua vema kutokubali kurubuniwa na makundi ya aina yoyote
au vyama vya siasa bali wanatakiwa kutumia nguvu zao walizonazo kwa wakati huu
ili kuwa chachu ya maendeleo hapa nchini
Aidha
alieleza kuwa wanasiasa wengi katika maeneo mengi Duniani upenda kuwatumia
vijana ili kutimiza adhima yao hata kama wao hawajui kile wanachokipigania wala
kuhoji ila kama vijana watajitambua umuhimu wao , uwezekano wa kushawishiwa
kuingia katika matende ya uvunjifu wa Amani hautawezekana kwani wengi kwa
kutofuata utaratibu uweza kupoteza maisha au kupata vilema vya kudumu
Nae Katibu
wa uvccm Kibondo James Rafael aliwataka vijana wa umoja huo kutojiingiza katika
makundi vya ulaji rushwa na matendo yasiyofaa katika jamii ili kuendeleza
heshima ya chama hicho hasa wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika octoba mwaka huu Taarifa zaidi
Alieza kuwa
nchi hii imekuwa na changamoto nyingi ikiwa pamoja na kukosa baadhi ya viongozi
waadilifu ambao wamekuwa ni vikwazo katika kuwaletea maendeleo wananchi wao
kutegemeana na maeneo husika akitaja
hatua kuwa hatua ambayo usababishwa na wananchi kufanya uchaguzi kwa kukomoa
upande flani au kutumia jaziba ushabiki
na kuwaweka watu wasiofaa kwenye nyadhifa za kuwaatumikia watanzania na
kuwaacha wakilalamika
Katika
uchaguzi huo nafasi zilizokuwa zikipigania ni Katibu, Mjumbe wa mkutano mkuu wa
mkoa,wajumbe wa kamati ya utekelezaji na Baraza la umoja wa vijana ccm ambapo
waliopata nafasi hizo wote kuhakikisha wanafuata taratibu na kanuni umoja huo
na chama kwa ujumla ili kuondokana na kukipaka matope na kupoteza Imani kwa
wafuasi na walio nje ya chama
Maoni
Chapisha Maoni