Kibondo;Migogoro mingi na mikubwa yakugombania ardhi hapa nchini, imetajwa kusababishwa na uelewa ndogo kwa jamii juu ya matumizi na umiliki wa ardhi kwa kuzingatia utawala wa sheria
Washiriki wa semina juu sheria ya umiliki wa ardhi |
Nichoraus Ntiayagila mwanasheria Halmashauri ya Kibondo aliyekuwa mkufunzi katika semina hiyo |
Padre Andrea Kelemiye Parokia ya Mabamba |
Kibondo;Migogoro
mingi na mikubwa yakugombania ardhi hapa nchini, imetajwa kusababishwa na
uelewa ndogo kwa jamii juu ya matumizi na umiliki wa ardhi kwa kuzingatia
utawala wa sheria
Kutokana na hali hiyo, ili kuzuia na kupunguza malumbano
katika jamii, Kanisa Katholic Jimbo la Kigoma jana limeamu kutoa mafunzo kwa muda siku mbili kwa
wenyeviti , Watendaji wa kata na vijiji ili waweze kufahamu sheria ya umiliki
wa ardhi kama anavyoleza Padre Andrea Kalemiye kutoka Parokia ya Mabamba
wilayani Kibondo
‘’Kumekuwepo na migogoro
ambayo haina sababu na kupelekea watu
kusababishiana madhala ya kuuwana na kuitilafiana kati ya Mtu na mwenzake Mtu
na Taasisi hivyo tumeona tuweke mafunzo haya ili watu hasa viongozi wa Vijiji
wafahamu jinsi ya kutatua migogoro ya ardhi kisheria ailisema Kelamiye ‘’Paroko
Parokia ya Mambamba
Mkufunzi wa mafunzo
hayo Nichoraus Ntiyagila ambaye ni mwanasheria Halmashauri ya Kibondo, amesema
kutoka na viongozi wengi katika ambako ndiko jamii kubwa iliko hasa kwenye
mabaraza ya ardhi kumekuwa kukifanyika mambo yasiyo hama kwa makusudi au kwa
kutokujua na kusisitiza kuwa kila mtuapaswa kujua anatakiwa kufuata sheria
Aidha Ntiyagila alisema kuwa maeneo mengi Vijijini na maeneo yenye madini watu wamekuwa wakishindwa
kuafahamu ardhi ni nini na ni vitu gani vinavyo
sababisha ardhi na ni vitu gani ambavyo mtu anaruhusiwa kisheria
kuvimiliki yeye binafi si kama madini, Mafuta na Gesi ambapo haijuishwi katika
ardhi na kuanza kugombania wengine kwa kufahamu au kwa makusudi
Nao baadhi ya washiriki walisema kuwa wameongezewa maarifa
hasa kwa maswala ya utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa kuzingatia sheria kwa kuwa
tangu wamechaguliwa hawakuweza kupata maelekezo kama hayo na kuahidi kutumia
elimu hiyo mara watakapo kuwa katika vituo vyao vya kazi
Wilaya ya Kibondo ilianzishwa mwaka 1954 na ilipofika mwaka
2012 baadhi ya maeneo yake yaligawanywa na kuunda wilaya mpya ya Kakonko, ambapo
kwa sensa ya mwaka 2012 wilaya ya kibondo ilikuwa na Idadi ya Watu 261,331 huku
tangu kuanzishwa kwake hadi mwaka huu ilikuwa ina hati 60 tu za watu wanaomiliki ardhi
Nae Mbunge wa Jimbo la Mhambwe wilayani humo Atashasta
Nditiye yeye amongeza kuwa ili kuondoa
migogoro ya ardhi ndani ya jamii serikali ina mpango wa kupima ardhi na kutoa
hati kwa wamiliki kwa nchi nzima nzima na kibondo ikiwemo hatua itakayoondoa
malumbano na kuwafanaya wananchi kunufaika na ardhi yao
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni