Uvinza;Halmashauri ya wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma inakabiliwa na ukosefu wa hospitali ya wilaya hiyo jambo linalopelekea wananchi kusafiri umbali mrefu kutafuta matibabu katika hospitali nyingine ikiwemo hospitali ya rufaa ya mkoa huo - Maweni.

Uvinza;Halmashauri ya wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma inakabiliwa na ukosefu wa hospitali ya wilaya hiyo jambo linalopelekea wananchi  kusafiri umbali mrefu kutafuta matibabu katika hospitali ny
ingine  ikiwemo hospitali ya rufaa ya mkoa huo - Maweni.

Hayo yalibainishwa juzi na mkuu wa wilaya hiyo Mwanambua Mlindoko mara baada ya kupokea Vifaa tiba na Magodoro vyenye thamani ya milion 5 kutoka Benki ya NMB na kusema ukosefu wa huduma Bora za afya wilayani humo, bado ni changamoto kubwa na kwa serikali imejipanga kuhakisha inabiliana nazo haraka iwezekanavyo

Alisema hivi sasa wanarekebisha Kituo cha Afya cha uvinza kwa kuongeza majengo na vifaa vingine ili kiweze kutumika kama Hospitali ya Wilaya, huku wakifanya maandalizi ya ujenzi wa hospitali ambapo wanataraji kuijenga katika eneo la Lugufu ambako walipata kiwanja kwa ajili ya kujenga hospitali hiyo.

Kwa upande wake meneja wa NMB Tawi la Kigoma Joventus Lukonge alisema benki hiyo imeamua kutoa msahada huo ilikuunga mkono juhudi za serikali kuboresha huduma za afya nchini na kuondoa adha kwa wananchi
Baadhi ya wananchi walishiriki zoezi hizo,ambao ni Agnes Makala na 

Hellen Jacob, ambao walipongeza uamuzi huo, na kueleza kutokana na jiografia ya wilaya hiyo wananchi wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa kufuata matibabu
‘’katika wilaya hii wapo wengi wanaoishi maporini kwa ajili ya shugumbali mbali kama kilimo hivyo linapotokea tatizo kama la ugonjwa, wengine ufia njiani wakipelekwa kupelekwa kupatiwa matibabu hasa wajawazito’’ alisema Agnes.

Wilaya ya Uvinza ina Zahanati 45 na Vituo vya Afya 5 haina hospitali hatua inayosababisha watu wengi kutembea umbali wa kilomita 90 kufuata matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa kigoma

Wilaya ya Uvinza ilianzishwa mwaka 2012 na ina ina idadi ya watu 383,640 kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2012 lakini hadi sasa haijapata hospitali ya Wilaya

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao