Uvinza;Halmashauri ya wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma inakabiliwa na ukosefu wa hospitali ya wilaya hiyo jambo linalopelekea wananchi kusafiri umbali mrefu kutafuta matibabu katika hospitali nyingine ikiwemo hospitali ya rufaa ya mkoa huo - Maweni.
Uvinza;Halmashauri
ya wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma inakabiliwa na ukosefu wa hospitali ya wilaya
hiyo jambo linalopelekea wananchi kusafiri umbali mrefu kutafuta matibabu
katika hospitali nyingine ikiwemo hospitali ya rufaa ya mkoa huo -
Maweni.
Hayo yalibainishwa
juzi na mkuu wa wilaya hiyo Mwanambua Mlindoko mara baada ya kupokea Vifaa tiba
na Magodoro vyenye thamani ya milion 5 kutoka Benki ya NMB na kusema ukosefu wa
huduma Bora za afya wilayani humo, bado ni changamoto kubwa na kwa serikali
imejipanga kuhakisha inabiliana nazo haraka iwezekanavyo
Alisema hivi
sasa wanarekebisha Kituo cha Afya cha uvinza kwa kuongeza majengo na vifaa
vingine ili kiweze kutumika kama Hospitali ya Wilaya, huku wakifanya maandalizi
ya ujenzi wa hospitali ambapo wanataraji kuijenga katika eneo la Lugufu ambako
walipata kiwanja kwa ajili ya kujenga hospitali hiyo.
Kwa upande
wake meneja wa NMB Tawi la Kigoma Joventus Lukonge alisema benki hiyo imeamua
kutoa msahada huo ilikuunga mkono juhudi za serikali kuboresha huduma za afya
nchini na kuondoa adha kwa wananchi
Baadhi ya
wananchi walishiriki zoezi hizo,ambao ni Agnes Makala na
Hellen Jacob, ambao
walipongeza uamuzi huo, na kueleza kutokana na jiografia ya wilaya hiyo
wananchi wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa kufuata matibabu
‘’katika
wilaya hii wapo wengi wanaoishi maporini kwa ajili ya shugumbali mbali kama
kilimo hivyo linapotokea tatizo kama la ugonjwa, wengine ufia njiani
wakipelekwa kupelekwa kupatiwa matibabu hasa wajawazito’’ alisema Agnes.
Wilaya ya
Uvinza ina Zahanati 45 na Vituo vya Afya 5 haina hospitali hatua inayosababisha
watu wengi kutembea umbali wa kilomita 90 kufuata matibabu katika hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa kigoma
Wilaya ya
Uvinza ilianzishwa mwaka 2012 na ina ina idadi ya watu 383,640 kwa mujibu wa
sensa iliyofanyika mwaka 2012 lakini hadi sasa haijapata hospitali ya Wilaya
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni