UKARABATI WA MELI YA MV LIEMBA MKOANI KIGOMA WAFIKIA 64%

 











Dkt Rashid Chuachua Mkuu wa Wilaya ya Kigoma





Serikali ya Tanzania yaendelea kukarabati Meli ya Mv Liemba ambayo imekuwa ikifanya shughuli zake katika Ziwa Tanganyika na zoezi hili linafanyika Mkoani Kigoma [engo ikiwani kuboresha huduma za usafiri wa Majini kwa Wananchi wa Mwambao wa Ziwa Tanganyika na Nchi jirani za Burundi Congo DRC na Tanzania

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro, amemshukuru Rais wa JamhurI ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha zaidi ya Shilingi Bilioni 32 kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa Meli ya Kihistoria ya Mv.Liemba.

Shukrani hizo za Mkuu wa Mkoa Balozi Simon Sirro kwa Rais, zimetolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua, wakati alipomwakilisha kwenye mapokezi ya Injini mbili zilizofika kwa ajili ya kukamilisha ukarabati mkubwa wa Meli ya Mv.Liemba katika Bandari ya Kigoma.

Amesema hatua hiyo inaashiria historia mpya kwa wana Kigoma kwenye sekta ya usafiri na usafirishaji katika Ziwa Tanganyika, baada ya miaka kadhaa ya kusimama kwa Meli ya Mv.Liemba bila kutoa huduma.

Meneja Mradi wa Ukarabati wa Meli ya Mv. Lemba Mhandisi Elias John Kivala, ukarabati wa meli hiyo umefikia asilimia 64%, na kwamba mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Julai mwaka huu.

Kwa upande wao Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Sadick Kibwana Kadulo, pamoja na Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Musa Maulid, wamesema meli hiyo ni mkombozi kwa wananchi wa Kigoma kwenye masuala ya usafiri na uchumi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

KUHITIMISHA UCHUKUAJI FOMU KINYANG'ANYIRO CHA UBUNGE JIMBOLA MUHAMBWE CCM