KIBONDO YAENDELEZA KAMPENI KUUNGANISHA WATOTO WANAOISHI MITAANI NA FAAMILIA ZAO NA WENGINE KURUDISHWA MASHULENI

 



Aneth Kolman Mkuu wa Dawati la Jinsia Jeshi la Polis Kibondo

Sophia Gwamagobe Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma

Lukas Lazaro mwakilishi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Kibondo

Skola Kachiila Mkazi wa Kibondo

Elias Jackson Mkazi wa Kibondo

Kuendelea kuwepo Watoto wanaofanya kazi na kuishi mitaani, hali hiyo imetajwa kuchochewa na baadhi ya Wazazi kutumia ukali zaidi katika kuwakanya, migogoro ya familia, umasikini na utukutu wa watoto wenyewe mambo hayo hupelekea kutoroka katika familia na kuishi mitaani

Wengi wa Watoto hao wanapoingia Mitaani huanza kufanyabiashara za kuokota na kuuza chupa za plastic na Vyuma chakavu na wengine kazi za majumbani na wanaokosa shughuli hujuhusisha na udokozi hatua ambayo ni hatari kwa maisha yao maana wengi wao ni wanakuwa na umri mdogo

Hayo yamebainishwa katika maadhimisho ya Mtoto anaeishi na kufanya kazi mitaani ambapo Afisa ustawi wa jamii wilaya ya Kibondo Kigoma, Sophia Gwamagobe ameeleza kutokana hali hiyo watoto huroka majumbani kuingia mitaani na kufanya kazihatarishi

 Aneth Kolman Mkuu wa Dawati la Jinsia Jeshi la Polisi Kibondo yeye amesistitiza umuhimu wa wazazi kutimiza makujukumu ya malezi huku akiwataka Wadau kulitazama kundi hili kwa jicho la pekeeili kuvinusuru vizazi vya vya sasa na vijavyo wengi wanakosa masomo na maadili kwa ujumla

Maadhimisho yanalenga kujenga uelewa katika jamii ili kupunguza wimbi la Watoto wanaoishi Mitaani jamii ikitakiwa kutambua suala zima la majukumu ya malezi, huku Watoto wakitakiwa kuacha utukutu na kuwatii wazazi, ameeleza hayo Lukas Lazaro akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kibondo katika maadhimisho hayo

‘’Nyinyi Watoto baadhi yenu mnajisababishia matatizo kwasababu wengine mmetoroka katika familia bila sababu ila tu mliamua kujiunga na makundi mkaanza tabia zisizo rafiki katika familia zenu na mnapoonywa wengine mnataka kujidhulu kimwili, maana hata wazazi wanapowarekebisha, huo ni upendo na uchungu kama wazazi wenu sasa nawashauri mjiepushe na tabia zisizofa muwatii wazazi kwa mambo mema wanayo waelekeza’’ amesema Lukas

Elias Jackson na Skola Kachiila ni baadhi ya Wazazi ambao wanaeleza kuwa hakuna mzazi anaefurahi Mtoto kuishi mitaani changamoto ni utukutu wa Watoto na baadhi ya Wazazi kukwepa majukumu na kuomba sheria zitumike kwani hali hiyo inaweza kuendeleza uwepo wa makumdi mabaya ya kiharifu

Pamoja na mambo mengine Wilaya ya Kibondo imeanza kuondoa watoto hao mitaani na kuwaunganisha na familia zao na wale ambao wameacha masomo wanarudishwa mashuleni na katika miezi miwili wameunganishwa watoto nane katika familia,  huku ufutiliaji ukiendelea kutambua kila motto anakotokea

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

40 CHADEMA KIBONDO WAJIONDOA

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu