KATIKA KUKABILIANA NA MAJANGA YA MOTO SERIKALI IMETOA GARI LENYE MTAMBO WA KUZIMIA MOTO KATIKA WILAYA YA KIBONDO

 






Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma imepokea gari (mtambo) utakaosaidia katika kukabiliana na majanga ya moto yanapotoke

Uzinduzi wa mtambo umefanyika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kibondo ambapo mkuu wa wilaya hiyo Kanali Aggrey Magwaza amesema mtambo huo utasaidia kwa kiasi kikubwa hasa pale zitakapotokea changamoto za ajali za moto

Aidha ameagiza uongozi wa halmashauri chini ya mwenyekiti wa halmashauri Bw. Alex Baragomwa kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa zimamoto katika upatikanaji wa maji, mafuta na matengenezo ya mtambo huo ili uendelee kutoa huduma katika hali ya ubora

Awali kaimu Kamada wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Kigoma Mrakibu masaidizi Michale Maganga amesema imani yake ni kwamba, kuwepo kw amtambo huo kutawafanya wananchi wa wilaya ya Kibondo wawe salama zaidi dhidi ya majanga ya moto

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo Bw. Alex Baragomwa pamoja na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wa wilaya hiyo Bw. Hamisi Tahiro wameomba elimu izidi kutolewa hasa katika kuepuka ujenzi holela unaoweza kuepelekea kushindwa kufanyika kwa zoezi la kuzima moto kwa kukosa mahali pa kupitisha mtambo huo.

 

 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

40 CHADEMA KIBONDO WAJIONDOA

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu