ONGEZEKO LA IDADI YA WATU NI TATIZO LA KIMATAIFA

 


Ongezeko la idadi ya watu Duniani, ni tatizo la kimataifa na na linatajwa kusababisha changamoto mbalimbali za Kibinadamu japo uwepo wa Binadamu katika uso wa Dunia ni jambo la muhimu

Kwa mujibu wa makadirio ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa kupitia Divisheni ya Idadi ya Watu ya UN (UN DESA Population Division), ni kwamba  kufikia mwezi Julai 2025, dunia ilikadiriwa kuwa na zaidi ya watu bilioni 8.1.

Nchi zenye Idadikubwa  ya Watu Duniani ni  ni China na India  ambapo katika Nchi ya India kuna Watu wapatao 1,339,180,127 na China ikiwa na Idadi ya Watu 1,409,517,397 huku Bara la Afrika likiwa na Watu billion 1.58

Kila uchao Wanadamu wamekuwa wakiongezeka kwa kasi huku Dunia ikiwa pale pale na mahitaji ya lazima  ya kibindamu kama ardhi  vikiwa haviongezeki  na huduma za Afya, Maji, Chakula na makazi,  upatikanaji wake ukiwa ngumu na kuufanya ulimwengu kuwa katika hali ya hatari ya kukumbwa na Majanga ya Kibinadamu

Kutokana na hali hiyo, kila ifikapo Julai 11 kila mwaka Dunia uadhimisha Siku ya Idadi ya Watu Duniani,  lengo la kuadhimisha siku hii ni kuongeza uelewa kuhusu masuala yanayohusiana na ongezeko la watu duniani, ikiwa ni pamoja na changamoto za maendeleo endelevuili kwa ajili  kuboresha  upatikanaji wa huduma za Kijamii na matumizi ya  rasilimali na kuepuka athari za kijamii na kimazingira


Maadhimisho haya hutumika pia kuhamasisha nchi wanachama na mashirika mbalimbali kushirikiana katika kupanga sera zinazolenga kuboresha maisha ya watu, hasa katika maeneo yenye ongezeko kubwa la idadi ya watu au changamoto za kijamii na kiuchumi zinazotokana na idadi kubwa ya watu.

 Tanzania kunakokadiriwa kuwa na zaidi ya Watu  zaidi ya Milion 61 licha ya ongezeko la Idadi ya Watu, Elimu inahitajika kutunza Kilichopo kwa ajili ya Vizazi vilivyopo na vijavo kama matumizi bora ya ardhi na utunzaji wa miundombinu kama Vituo vya kutolea huduma za afya, Elimu Barabara Maji na mingineyo mingi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

KATIKA KUKABILIANA NA MAJANGA YA MOTO SERIKALI IMETOA GARI LENYE MTAMBO WA KUZIMIA MOTO KATIKA WILAYA YA KIBONDO