Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2015

Wastaafu wa kada mbalimbali hapa nchini wametakiwa kuwa chachu ya maenedeleo kwa kuwasadia wale walioko makazini kwa kutoa ushauri juu ya vikwazo walivyo kutana navyo kazini ikiwamo, na mafanikio kwa ujumlana namna ya kufanya kazi kwa welediNdyaki Majo katibu cwt Kibondo

Picha
Wastaafu wa kada mbalimbali hapa nchini wametakiwa kuwa chachu ya maenedeleo kwa kuwasadia wale walioko makazini kwa kutoa ushauri juu ya vikwazo walivyo kutana navyo kazini ikiwamo, na mafanikio kwa ujumlana namna ya kufanya kazi kwa weledi Wito huwo  umetolewa na Katibu wa chama cha walimu wilaya kibondo Bw,Ndyaki Majo wakati wa hafra fupi ya kuwaaga walimu wastaafu iliyofanyika kwenye ukumbi wa chama hicho mjini kibondo. Majo amesema kuwa hivi sasa taaluma ya ualimu imejumuisha vijana  wengi ambao wanapangiwa kufanya kazi katika maeneo mengi ambao wanahitaji maelekezo waweze kupata ufanisi katika utendaji kazi hivyo, kama ni kustaafu ni kwa mujibu wa taratibu tu  lakini mchango wao bado unahitajika Nae mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya kibondo Tilimio Nzigo, amesema kuwa lengo la kutoa mkono wa kwaheri kwa wastaafu, ni kutambua  mchango wao walioutoa kwa umma, na kuongeza kuwa chama kinatambua kuwapo kwa changamoto zinazoendelea kuwakabili walimu na kitaendele

Wadau wa maendeleo ya jamii na mashirika mbalimbali na serikali kwa ujumla wametakiwa kuyaangalia kwa jicho la huruma makundi ya walemavu waishio vijijini kwani baadhi mahitaji yao ni makubwa kulingana na viwango vya ulemavu

Picha
Muhingo Mwemezi Kakonko Wadau wa maendeleo ya jamii na mashirika  mbalimbali na serikali kwa ujumla wametakiwa kuyaangalia kwa jicho la huruma makundi ya walemavu waishio vijijini kwani baadhi mahitaji yao ni makubwa kulingana na viwango vya ulemavu Akiongea katika Kijiji cha Malenga wilayani Kakonko Mkoani Kigoma Mbunge wa jimbo la Buyungu Kasuku Bilago amesema kuwa jamii zinaishi vijijini hazina uwezo wa kuwasidia ipasavyo walemavu ikilinganishwa na vipato vyao kiuchumi hatua inayopelekea wengi wao kukata tamaa  Hata hivyo Bilago alitoa msahada wa baiskeli nne zenye Magurudumu manne, zenye thamani ya tsh milion mbili kwa baadhi ya walemavu wa miguu wanaotembea kwa kujivuta ili ziweze kuwasaidia kwenda sehemu moja hadi nyingine na kuiomba serikali kuelekeza nguvu zake kwa makundi hayo yanayoishi vijijini  Baadhi ya  walionufaika na msahada huo ambao ni Chubwa Maasbo Mkazi wa malenga na Erasmus Bilunda mkazi Kasuga wameeleza changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo k

Wakazi wa Kijiji cha Kikulazo Kata ya Lugenge, wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wameiomba serikali kulishawishi shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa matifa UNHCR kujenga kituo maalum cha kuwapokelea wakimbizi toka nchini Burundi wanaoendelea kukimbia machafuko ya kisiasa nchini mwao, ili kunusulu afya za wanakijiji wanaishishi mipakani baada ya raia hao kuanza kukimbia na kukosa sehemu maalum ya kufikia hatimae kuchafua mazingira

Picha
Wakazi wa Kijiji cha Kikulazo Kata ya Lugenge, wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wameiomba serikali kulishawishi shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa matifa UNHCR kujenga kituo maalum cha kuwapokelea wakimbizi toka nchini Burundi wanaoendelea kukimbia machafuko ya kisiasa nchini mwao, ili kunusulu afya za wanakijiji wanaishishi mipakani baada ya raia hao kuanza kukimbia na kukosa sehemu maalum ya kufikia hatimae kuchafua mazingira Waliliiambia gazeti hili kijijini hapo,jana kuwa hivi sasa hali ni mbaya katika kijiji hicho kwani kimekuwa kikipokea wakimbizi wengi wanaokingia Tanzania kwa ajili ya kuomba hifadhi na kwakuwa hakuna eneo maalum la kuwapokelea lilitengwa, ufikishiwa katika gala la la kutunzia vyakula  hali ina inayopelekea kjisadia hovyo, pia na huduma za kijamii hazipo Beatus Mpera, ambae ni mkazi wa kijiji hicho ameleza kuwa hofu yao kubwa ni kutokea magonjwa ya mlipuko na mengineyo katika maeneo hayo na kuongeza kuwa huduma za muhimu kama ameneo ya k

Miili zaidi ya 34 imepatikana katika barabara za mji mkuu wa Burundi huku machafuko yakiendelea, huku jeshi likisema watu 87 waliuawa Ijumaa. Mwandishi wa BBC ameona maiti 21 katika mtaa mmoja wa Bujumbura na maafisa wa serikali wamesema kuna miili mingine 13.

Picha
Miili zaidi ya 34 imepatikana katika barabara za mji mkuu wa Burundi huku machafuko yakiendelea, huku jeshi likisema watu 87 waliuawa Ijumaa. Mwandishi wa BBC ameona maiti 21 katika mtaa mmoja wa Bujumbura na maafisa wa serikali wamesema kuna miili mingine 13. Maiti nyingi zinaonekana kuwa za vijana waliouawa kwa kupigwa risasi, baadhi wakiwa wamefungwa mikono yao ikiwa pamoja mgongoni. Miili hiyo imepatikana siku moja baada ya watu wenye silaha kushambulia maeneo matatu ya jeshi. Jeshi la Burundi limesema watu 87 waliuawa kwenye mapigano ya Ijumaa, wanane kati yao wakiwa maafisa wa usalama. Machafuko yameendelea kutatiza Burundi tangu kutibuliwa kwa jaribio la kupindua serikali mwezi Mei na maandamano yaliyofanyika kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa mara nyingine, wazo alilotangaza Aprili. Bw Nkurunziza alishinda uchaguzi uliofanyika Julai.

Viongozi wanaoaminiwa na kupewa dhamana ya kuwaongoza wananchi wametakiwa kujijengea mazingira ya uaminifu kwa kutenda yale yanayostaili na kuenenda kwa kufuata sheria taratibu na kutimiza viapo vyao ili kuondoa kukata tamaa kwa wananchi wao

Picha
Viongozi wanaoaminiwa na kupewa dhamana ya kuwaongoza wananchi wametakiwa  kujijengea mazingira ya uaminifu kwa kutenda yale yanayostaili na kuenenda kwa kufuata sheria  taratibu na kutimiza viapo vyao ili kuondoa kukata tamaa kwa wananchi wao Erick Marey Hakimu wa wilaya ya Kibondo wakati wa kuwahapisha madiwani Halmashauri ya Kakonko Peter Toyima Dc Kakonko Akizungumza juzi, katika uzinzinduzi wa Baraza la Halmashauri la walaya ya Kakonko Mkoani Kigoma,  Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Kibondo Erick Marey wakati wa kuwahapisha madiwani alisema kuwa kiapo ni ishara ya utii kwa mlengwa hivo ni lazaima kifuatwe kwa kuyatenda yale kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi na kinyume na hasipofuata taratibu hizo anastaili kufikishwa katika vyombo vya sheria ili kuwajibishwa Katika kikao hicho mara baada ya kuhapishwa madiwani hao, ulifanyika uchaguzi wa mwenyekiti  wa halmashauri na makamu wake ambapo Juma Maganga kata ya kakonko, alipata kura 12  huku mpizani wake Eliya

Wakulima na wafugaji wakijiji cha Gwanumpu Kata ya Gwanumpu wilayani kakonko mkoani kigoma wameitaka serikali kuingilia katimgogoro uliopo kati ya wafugaji na wakulima hali ambayo huwafanya kulipiziana visasi kilawakati

Picha
Wakulima na wafugaji wakijiji cha Gwanumpu Kata ya Gwanumpu wilayani kakonko mkoani kigoma wameitaka serikali kuingilia katimgogoro uliopo kati ya wafugaji na wakulima hali ambayo huwafanya kulipiziana visasi kilawakati. Mtondo Mtondo mkulima wa Kijiji cha Gwanumpu Bw, Toyi Slivester Diwani kata ya Gwanumpu -Wakiongea katika mkutano wa hadhara jana uliofanyika kijiji hapo, wamesema kwasasa wakulima na wafugaji hawaelewani kwa kile wanachokidai kuwa kila mmoja huona yuko sahihi katika eneo  ambalo linadaiwa kutengwa kwa ajili ya malisho na uonekana kuwa na rutuba nzuri pamoja na nyasi nzuri za kulishia mifugo. Bw.Godwini George ni mmoja wa wafugaji anasema eneo hilo awali lilitengwa kwa ajili ya wafugaji lakini kwasasa wakulima wamevamia maeneo hayo huku Bw.Mtondo Danieli ambae ni mkulima akidai kuwa amefanya shughuli za kilimo katika maeneo hayo kwa muda miaka sabana hakuna aliyewahi kumueleza kuwa eneo hilo ni kwa ajili ya malisho ya mifungo Aidha Mto

Jamii wilayani Kibondo imetakiwa kufuata taratibu za usafi kwa kutokuuza na kula, kiholela vyakula kama mbogamboga na matunda yaliyomenywa ili kuepuka magonjwa ya mlipuko yatokanayo na uchafu

Picha
Mwemezi Muhingo Kibondo Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma Bi. Ruth Msafiri, amepiga marufuku watumishi wa serikali Wilayani humo kuacha kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo amesema linaweza kukwamisha ufanisi katika shughuli za umma Wilayani Kibondo. Bi. Msafiri aliyasema hayo jana katika kikao kilichowahusisha   watumishi wa idara ya afya wilayani kibondo, wakiwemo viongozi kutoka taasisi mbalimbali wilayani humo, lengo ikiwa ni kujadili namna ya kuweka tahadhari ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu, endapo utajitokeza wilayani humo. Aidha alieleza kuwa kila mtumishi wa serikali anapaswa kuwajibika kikamilifu katika nafasi yake, ili  kuhakikisha kuwa dalili za ugonjwa huo zinakomeshwa kikamilifu, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha zoezi la usafi wa mazingira wilayani humo linafanyika kila siku za aihamisi, kwa kushirikisha watumishi wote wa serikali pamoja na wananchi. Hata hivyo amekemea vitendo vya baadhi ya watumishi wa serikali kuamua kujipa mapumziko y

Ukakamavu ni jambo la muhimu sana katika maisha ya Binadamu kwani uujenga na kuuweka sawa mwili

Picha
Hao ni baadhi ya vijana wakiwa kwenye Gwaride la kuhitimu  katika moja ya mafunzo ya awali ya kijeshi katika kikosi cha 824 kj Kanembwa Jkt kilicho wilayani Kakonko moani Kigoma Mafunzo hayo yalifungwa rasmi na Mkuu wa mkoa wa Kigoma Bw, Issa Machibya, kwa kuwakilishwa na mkuu wa wilaya kakonko Peter Toyma na kuwapandisha kutoka daraja la clut na kuwa service Girls na Boys huku jumbe mbalimbali zikitolewa kwa ajili ya kuwaasa kufuata taratibu za nchi na kutimiza viapo vyao Vijana hao ni kwa mujibu wa sheria, hususa ni wale waliomaliza  kidato cha sita 2015 katika shule mbalimbali za sekondari hapa nchini  na kundi hilo kupewa jina la Oparation Kikwete Mkuu wa Kikosi hicho Luten Conal Amos Gerad na viongozi wengozi wengine wakiwemo maafisa wa jeshi hilo walitoa jumbe mbalimbali kwa jamii ya  kitanzania juu ya kulifahamu na kuthamini kazi zake kwani lipo kwa mujibu sheria za nchi na ni kwa ajili ya watanzania wote, huku vijana wenyewe wakitoa shukrani zao wa wazazi na serikali kwa

Ubelgiji imewashauri raia wake kuondoka Burundi, huku Muungano wa Ulaya nao ukipunguza maafisa wake wanaohudumu huko kutokana na kuongezeka kwa machafuko

Picha
Balozi wa EU nchini humo Patrick Spirlet amesema hatari ya kutokea mapigano zaidi imeongezeka. Hayo yamejiri huku idara ya Amani ya Usalama ya Muungano wa Afrika ikikutana mjini Addis Ababa kujadili mpango wa kutuma walinda amani nchini humo. Kamishna wa Amani wa AU Smail Chergui amesema atatuma maafisa nchini Uganda kuandaa mazungumzo kati ya Rais Nkurunziza na upinzani. Watu zaidi ya 200 wameuawa tangu Aprili Rais Nkurunziza alipotangaza kuwa angewania urais kwa muhula wa tatu. Alishinda uchaguzi mwezi Julai. Mnamo Alhamisi, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja lilipitisha azimio lenye mapendekezo mengi yakiwemo uwezekano wa kutumwa kwa walinda Amani, na kuwekwa kwa vikwazo. Kiongozi mmoja wa upinzani nchini Burundi tayari ameuhimiza Umoja wa Mataifa kutuma walinda usalama nchini humo. Charles Nditije, mkuu wa kundi la upinzani la UPRONA, ameambia shirika la habari la Reuters kwamba wanafurahishwa na juhudi za UN kuhimiza mashauriano lakini wamevunjwa moy

Mamlaka ya safari za ndege nchini Urusi imepiga marufuku ndege za shirika la taifa la ndege la Misri kuhudumu Urusi, msemaji wa uwanja wa ndege Moscow amesema.

Picha
Safari za ndege kutoka Urusi hadi Misri tayari zilikuwa zimesimamishwa baada ya ndege ya Urusi kuanguka eneo la Sinai mwezi jana. Abiria wote 224 walifariki, wengi wao wakiwa raia wa Urusi. Shirika hilo la Egypt Air ndilo pekee lililokuwa limesalia likifanya safari kati ya mataifa hayo mawili. Vyombo ya habari Urusi zinasema shirika hilo limepigwa marufuku kuhakikisha linatimiza matakwa ya kiusalama. Kundi la Sinai Province, lenye ushirika na Islamic State, limedai kuhusika katika kuangusha ndege ya Metrojet nambari 9268, iliyokuwa ikitoka Sharm el-Sheikh kuelekea St Petersburg Urusi. Mataifa ya Magharibi yamesema kuna uwezekano mkubwa bomu lililipuka ndani ya ndege hiyo ikiwa angani, lakini Urusi na Misri zimesema ni mapema mno kuthibitisha hayo. Baada ya ajali hiyo, mataifa kadha, ikiwemo Uingereza, yalisitisha safari za ndege za kuingia na kutoka Sharm el-Sheikh, yakitaja wasiwasi kuhusu usalama. Ndege za Egypt Air ndizo pekee zilikuwa zinahudumu kati ya Misri na Uru

Maafisa wa polisi nchini Tanzania wamesema kuwa wanamzuia msaidizi wa aliyekuwa waziri mkuu wa taifa hilo Edward Lowassa ili kuchunguzwa kuhusiana na uraia wake.

Picha
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini humo,wamesema kuwa bwana Bashir Fenel Awale Ally ambaye amekuwa mtu muhimu katika kampeni za urais za bwana Lowassa atachunguzwa kuhusiana na stakhabadhi zinazotilia shaka kuhusu uraia wake. Kamanda maalum wa polisi katika eneo la Dar es Salaam, Suleiman Kova amewaambia waandishi wa habari kwamba stakhabadhi alizokamatwa nazo zinatatiza kuhusiana na taifa analotoka. Amesema kuwa wakati wa kukamatwa kwake mtu huyo alipatikana na cheti cha kuzaliwa kinachoonyesha kwamba alizaliwa tarehe 11 mwezi Julai mwaka 1969 mjini Dodoma. Kulingana na afisa huyo mshukiwa huyo pia alipatikana na pasipoti iliotoka jijini nairobi na ambayo inayoonyesha kwamba alizaliwa mjini humo mnamo tarehe 11 mwezi Julai mwaka 1969,akiwa na jina la Bashir Fenal Abdi Ally Awadhi . Mshukiwa huyo anayedaiwa kuwa mwanaharakati na mfuasi mkubwa wa chama cha upinzani Chadema alikamatwa nyumbani kwake huko Mikocheni. Kova amesema kuwa kuna ishara kwamba mshukiwa huyo ni r

Viongozi wa Muungano wa Ulaya wanatarajiwa kutoa mabilioni ya euro kwa mataifa ya Afrika kuyawezesha kusaidia kupunguza mzozo wa wahamiaji Ulaya.

Picha
Tume ya Muungano wa Ulaya imesema itatoa €1.8bn (£1.3bn) na inatarajia mataifa zaidi ya EU yaahidi pesa zaidi. Lengo la ufadhili huo ni kusaidia kusuluhisha matatizo ya kiuchumi na kiusalama ambayo huwafanya watu kutoroka mataifa ya Afrika. Aidha, zitatumiwa kuyashawishi mataifa ya Afrika kuwapokea watu ambao wamenyimwa hifadhi Ulaya. Ahadi hiyo inatarajiwa kutolewa kwenye mkutano mkuu kuhusu wahamiaji unaofanyika Malta, na ambao ulipangwa baada ya meli iliyobeba wahamiaji kuzama Libya mwezi Aprili. Watu 800 walifariki Watu 150,000 wamevuka bahari ya Mediterranean kutoka Afrika mwaka huu, wengi wakitua Italia na Malta. Hata hivyo, mtazamo wa EU umebadilika tangu Aprili na kuangazia zaidi wakimbizi wanaotoka mashariki na hasa Syria, ambao wanawasili kwanza Ugiriki na kuvuka hadi Uturuki kisha kuelekea kaskazini kupitia bataifa ya Balkan. Zaidi ya viongozi 60 kutoka Afrika na Ulaya, akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, wanakutana Valletta, Malta kwa mkutano huo mkuu

Wataalamu wa afya wanasema mpango wa chanjo kwa umma dhidi ya homa ya uti wa mgongo barani Afrika umepata mafanikio makubwa.

Picha
Zaidi ya watu milioni mbili walipata kinga dhidi ya maradhi hayo katika nchi zipatazo 16 barani Afrika, kutoka Gambia mpaka Ethiopia. Shirika la Afya Duniani limesema katika kipindi cha mwaka 2013 kulikuwa na wagonjwa wanne tu, katika bara hilo ambalo awali liliweka rekodi ya kuwa na maelfu ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo, kila mwaka. Kampeni ya kupambana na ugonjwa huo ilianza mwaka 2010. Kinga dhidi ya uti wa mgongo

Iran imenunua silaha kali ya ulinzi dhidi ya ndege za kivita na makombora kutoka Urusi.

Picha
Mtambo huo wa S-300 unauwezo mkubwa sana na yanaweza kudungua ndege na makombora yakiwa umbali wa kilomita 300. Mtambo huo wa S-300 unauwezo mkubwa sana na yanaweza kudungua ndege na makombora yakiwa umbali wa kilomita 300. Hii si mara ya kwanza kwa Urusi kufanya makubaliano haya na Iran. Mwaka wa 2007 mataifa hayo yalikubaliana kuhusiana na mitambo hiyo ya ulinzi wa anga ila wakasitisha utekelezaji wake kufuatia marufuku iliyowekewa Iran kufuatia mipango yake ya kumiliki silaha za kinyuklia. Lakini punde baada ya kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya ununuzi wa silaha Iran sasa inapania kukamilisha mkataba huo. Mtambo huo wa S-300 ulitumika kwa mara ya kwanza wakati wa vita baridi na ulionekana kuwa na uwezo mkubwa wa kukabili ndege zaidi ya moja na makombora umbali wa kilomita 300. Mkurugenzi wa kampuni inayotengeneza silaha hiyo , Rostec,bwana Sergei Chemezov aliwaambia waandishi wa habari wa RIA kuwa kandarasi hiyo imeshatiwa sahihi. Add caption Urusi yaiuzia Ira

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameshutumu vikali viongozi wa Burundi kutokana na mauaji yanayoendelea nchini humo nakuonya kuwa huenda kukatokea mauaji ya halaiki

Picha
Bw Kagame ameshangaa ni vipi viongozi wa taifa hilo jirani "wanaweza kuruhusu wananchi wao kuuwawa kiholela". Rais Kagame alisema hayo Ijumaa, lakini matamshi yake hayakutangazwa hadi mwishoni mwa wiki, akionekana sana kumlenga Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza. Akizungumza kwa Kinyarwanda Rais Kagame alisema: ''Tazama nchi jirani kama Burundi, maisha yao yamesimama kabisa. Lakini sababu ni ipi? Wana historia inayofanana na yetu. Ila viongozi wao wapo kwa ajili ya kuua wananchi kuanzia asubuhi hadi jioni." ''Rais akajifungia sehemu isiyojulikana, hakuna anayejua sehemu alikojificha, hakuna anayezungumza naye, huyo anaongoza watu vipi?" alisema Bw Kagame, akihutubu katika hafla ya kuwatunuku Wanyarwanda waliosaidia kuwaficha na kuwaokoa Watutsi wakati wa mauaji ya kimbari 1994 pamoja na wanaharakati wanaotetea umoja na maridhiano miongoni mwa Wanyarwanda. ''Watu wanakufa kila siku, maiti zinabururwa barabarani. La kusikitisha ni k

Aston Villa 0-0 Man City

Picha
Amini usiamini Aston Villa wanapata alama moja muhimu kutoka kwa vinara wa ligi kuu ya Uingereza Manchester City. City walikuwa na mazoea ya kuchukua pointi zote tatu lakini sasa Villa wamepata alama yao muhimu. Na sasa wanavunja msururu wa kushindwa katika mechi 14. Kipa wa Aston Villa analazimika kufanya kazi ya ziada kuwanyima Man City bao Mpira umekwisha ! Mashambulizi yanachacha mbele ya lango la Aston Villa Manchester United wanafanya mashambulizi makali mbele ya lango la Villa. Loooooo Mpira kombora la Vincent Kompany linagonga mchuma Kona Manchester City wanapata kona muhimu lakini wapi 86:17 Aston Villa 0-0 Man City Kona kuelekea upande wa Manchester City Joe Hart ndiye anayeipangua mpira wa kutupwa na inakuwa kona. Aston Villa 0-0 Man City 86 :06 Charles N'Zogbia ameanguka chini baada ya kugongwa jicho kimakosa. 80 :00 Aston Villa 0-0 Man City Ngome ya Villa leo imeimarika. Inaonekana kocha mpya Remi Garde ameanza kufanya mabadiliko ya