Korea Kusini imetoa ombi la kutaka kufanyika mazungumo ya juu na Korea Kasuni tarehe 9 mwezi huu kujadili ikiwa kuna uwezekano wa kushiriki mashindano ya masimu wa baridi mwaka 2018. Hii ni baada ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kusema kuwa alikuwa anatafikiria kutuma timu kwenda Pyeongchang nchini Korea Kusini kwa mashindano hayo mwezi Januari.
Korea Kusini imetoa ombi la kutaka
kufanyika mazungumo ya juu na Korea Kasuni tarehe 9 mwezi huu kujadili
ikiwa kuna uwezekano wa kushiriki mashindano ya masimu wa baridi mwaka
2018.
Hii ni baada ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un
kusema kuwa alikuwa anatafikiria kutuma timu kwenda Pyeongchang nchini
Korea Kusini kwa mashindano hayo mwezi Januari.- Kim Jong-un: Kibonyezo cha silaha za nyuklia kiko kwenye meza yangu
- Korea Kaskazini: Vikwazo vipya ni kama vita
Mapema rais wa Korea Kusini alisema kuwa ameiona hiyo kama fursa ya kuboresha uhusiano ulioharibika kati ya nchi hizo.
Waziri wa mapatano wa Korea Kusini Cho Myoung-gyon alipendekeza Jumanne kuwa wawakilishi watakutana katika kijiji ya mapatano cha Panmunjon.
Kijiji hicho kilicho eneo lenye ulinzi mkali la DMZ mpakani ndipo mazungumzo kati ya nchi hizo yamekuwa yakifanyika.
- Urusi yadaiwa kupeleka mafuta Korea Kaskazini
- Marekani yawawekea vikwazo wataalamu wa makombora Korea Kaskazini
Mazungumzo ya mwsiho ya juu yalifanyika Disemba mwaka 2015 katika eneo la pamoja la viwanda la Kaesong.
Yalimalizika bila makubaliano yoyote na ajenga ya mazungumzo haikutangazwa.
CHANZO CHA HABARI HII NI BBC
Maoni
Chapisha Maoni