Serikali imesema inalenga ifikapo mwaka 2021 vijiji vyote hapa nchini vitakuwa visambaziwa nishati ya umeme ili kuondoa changamotombalimbali zinazowakabili wananchi ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi hasa katika maeneo ya Vijijini
Muhingo Mwemezi
Medad Kaleman Waziri wa Nishati na Madini |
Raymon Seya [Tanesco] |
Bangie Msofe[Rea] |
Kibondo
Serikali imesema inalenga ifikapo mwaka 2021 vijiji vyote
hapa nchini vitakuwa visambaziwa nishati ya umeme ili kuondoa
changamotombalimbali zinazowakabili wananchi ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi
hasa katika maeneo ya Vijijini
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati na Madini Medadi
Kalemani wakati wa uzindizi wa Rea awamu ya tatu uliofanyika kimkoa katikata ya
mabamba wilayani kibondo mkoani Kigoma ambapo amesema hadi hivi sasa vijiji
vilivyobaki ni 7873 Nchi nzima
Aidha Kalemani amewataka Watanzania kutokana na hatua hiyo ya serikali kupitia wizara ya
Nishati na Madini kuchangamkia fulsa hiyo kwa kuboresha miundo mbinu majumbani
ili waweze kupata huduma hiyo muhimu
Katika Uzinduzi huo mkuu wa Mkoa Kigoma Brigedia General
Mstaafu Emmanuel Maganga amemtaka Mkandarasi kufuata taratibu za makubaliano na kuwataka wakuu wa wilaya za mkoa huo kuhakikisha wanafuatilia hatua zote na mkandarasi anavyofanya kazi
Kwa upande wake
mwakilishi wa Mkurugenzi wa huduma za Kiufundi wa Taasisi ya wakala wa huduma
za umeme Vijiji Rea, Bengie Msofe, amesema atahakikisha kazi zina kwenda kama
zilivyopangwa na kuwaomba wananchi ushirikiano huku mwakilishi wa Mkurugenzi
Mkuu Tanesco Raymond Seya, akisema kuwa
watazingatia viwango vya ubora wa mradi
kama inavyotakiwa na wanakamilisha kwa wakati
Mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya umeme katika wilaya za
Kakonko na Kibondo ni wa thamani ya shilingi billion 25 fedha za kitanzania na
mkoa mzima mzima wa kigoma, thamani yake ni shilingi billion 60 hadi kukamilika
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni