Rais wa Marekani amewashutumu wahamiaji wanaoingia nchini humo kwa kuwatusi katika afisi yake ndani ya Ikulu ya Whitehouse.

Rais wa Marekani amewashutumu wahamiaji wanaoingia nchini humo kwa kuwatusi katika afisi yake ndani ya Ikulu ya Whitehouse.
''Kwa nini tunawaruhusu watu hawa kutoka mataifa 'machafu'"?
Rais Trump aliwaambia wabunge siku ya Alhamisi kulingana na gazeti la The Washington Post.
Tamko hilo lilidaiwa kuwalenga watu kutoka Afrika, Haiti na El Salvador.
Ikulu ya Whitehouse haikukana tamko hilo ambalo lilithibitishwa na vyombo vyengine vya habari.
''Wanasiasa fulani wa Washington hupendelea kupigania mataifa ya kigeni, lakini rais Trump atawapigania raia wa M arekani pekee,taarifa iliotoka katika msemaji wa Ikulu Raj Sha ilisema.
Iliendelea: Kama mataifa mengine ambayo yana wahamiaji wanaofaa kuwa nchini humo, rais Trump anapigania suluhu ya kudumu inazofanya taifa hilo kuwa thabiti kwa kuwakaribisha wale ambao wana mchango katika jamii ,hukuza uchumi wetu na kuingiliana na raia wa taifa letu.


Kamwe hatakubali mkakati wa muda mfupi ulio hafifu na hatari ambao unahatarisha maisha ya raia wa Marekani, mbali na kutowaruhusu wahamiaji wanaotaka maisha mazuri Marekani ijapokuwa kupitia njia halali.
Matamshi hayo ya rais Trump yanajiri huku wabunge kutika vyama vyote wakimtembelea kupendekeza mpango wa wahamaiji usiopendelea upande wowote.
Seneta wa Democrat Richard Durbin alikuwa akizungumza kuhusu vibali vya muda wa kuishi vinavyotolewa kwa raia wanaotoka katika mataifa yaliokumbwa na majanga, vita ama milipuko ya magonjwa, vilisema vyombi vya habari.
Kulingana gazeti la Washington Post , bwana Trump aliwaambia wabunge kwamba Marekani badala yake inachukua wahamiaji kutoka Norway, ambayo waziri wake mkuu alimtembelea rais Trump siku ya Jumatano.
Seneta Lindsey Graham, ambaye ni mwanachama wa chama cha Republian kutoka Carolina Kusini pia alikuwa katika mkutano huo lakini hakuweza kuzungumzia kuhusu matusi hayo yaliotolewa na rais Trum.
Gazeti la The New York Times liliripoti miaka mitatu iliopita kwamba bwana Trump alisema kuwa raia wa Haiti wote wana ''ukimwi'' wakati wa mkutano wa mwezi Juni kuhusu wahamiaji.
Na kufuatia matamshi hayo rais Trump hakusazwa katika mitandao ya kijamii.
Elijah Cummings, mbunge wa Democrat katika eneo la Maryland alichapisha ujumbe katika mtandao wa twitter akisema: Nayashutumu matamshi hayo yasiosameheka na yanayoshusha hadhi ya afisi ya rais.
Mbunge mwengine mweusi kutoka chama cha Democrat. Cedric Richmond, alisema matamshi ya bwana Trump ni dhihirisho tosha kwamba sera yake ya kuliimarisha taifa la Marekani ni sawa na kulifanya taifa la Marekani kuwa la watu weupe pekee.
Mia Love, raia wa chama cha Republican katika eneo la Utah ambaye pia ni mbunge wa pekee mwenye mizizi ya Haiti nchini Marekani amemtaka rais Trump kuomba msamaha kwa maneno hayo yalio na chuki na yenye kugawanya watu.
Muungano unaopigania haki za watu weusi NAACP ulimshutumu rais Trump kwa kuzidi kuegemea katika ubaguzi wa rangi.
Lakini Ikulu ya Whitehouse imepuuzilia mbalia shutuma hizo zinazomkabili rais.
Afisa mmoja wa Trump alinukuliwa na chombo cha habari cha CNN akisema: Ijapokuwa hili litawakasirisha watu wa Washington, wafanyikazi wanadhani kwamba matamshi hayo yanatokana na mizizi yake, sawa na matamshi yake dhidi ya wachezaji wa NFL waliopiga goti wakati wa kuimbwa kwa wimbo wa taifa.
Msemaji wa ubalozi wa El Salvador mjini Washington alikataa kuzungumzia kuhusu matamshi hayo.
Rais Trump ameyatusi mataifa ya Afrika , haiti na El salvador akidai ni machafu

Waandamanaji wanaopinga chuki ya rais Donald Trump dhidi ya wahamiaji

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao