TUNAVIJUA VIPAUMBELE VYETU? TUNASHIRIKI KUVITIMIZA?

TUNAVIJUA VIPAUMBELE VYETU? TUNASHIRIKI KUVITIMIZA?

Kila siku nasikia viongozi wetu wakiimba wimbo wa kuwainua wananchi wake kiuchumi. Mara viwanda. Mara kilimo ilichoboreshwa. Mara ufugani wenye tija. Ukisikia Rais anawahutubia mabalozi wetu wanaotuwakilisha nchi za nje, wimbo ni huo huo. Mabalozi wanaokuja kuziwakilisha nchi zao. Wanaambiwa angalieni fursa.
Utagundua haraka kuwa viongozi nao wamechoka kuongoza watu maskini. Wanataka wabadilike. 

Unatarajia kuwa kila mtu au taasisi itashiriki na kuchangia wimbo huo. Polisi barabarani hawatarajii kumsi9mamisha mwenye gari lililobeba nyanya na kuanza kumuuliza “mbona kuna mkwaruzo kwenye bonet”. Niliwahi kutembelea Rwanda myaka ya karibuni. Polisi walisimamisha gari lililobeba mazao yanayooza kama nyanya. Gari lilikuwa matairi yake yamekwisha. Polisi akamwambia dereva “ukifikisha mzigo wako kabadilishe matairi yako yameisha. Haya wahi”. 

Nilijua Polisi huyu anajua malengo ya Kagame. Si kuyajua tu bali anachangia kuyatimiza. Mifano tofauti ninayo kwa Polisi wa Magufuli.
Ninalotaka kujadili hapa ni vyombo vya habari.

Nina gazeti moja mkononi. Silitaji samahani. Ukitaka litafute. Ni la jana 22 January 2018.
1) Habari iliyopewa uzito ni ile ya mafao ya kujitoa na umbivu na umbichi wake. 
2) Ya pili ni Salaam za mbowe kwa tume ya Uchaguzi. 
3) Ya tatu ni Noa ilivyouna nusu ya familia. 
4) Mwisho ni habari za wazazi walio matatani kwa kumuoza mwanafunzi kwa mahari ya ng’ombe saba. 

5) Kuna picha kuuubwa ya waziri mkuu akiwa amemtembelea mama maria Nyerere.
Ninajishangaa kulinunua gazeti hilo ila huenda ili nijifunze jambo. Nikaangalia na kujiuliza hivi mwenye gazeti; mhariri wa gazeti na waandishi wao wote waliona nini kukosa habari japo moja inayoongelea maswala yanayolihusu taifa kwa sasa?

Kisanga nikafungua ndani. Nikakuta ukurasa wa pili kuna habari yenye kichwa kisemacho: FURSA KUPATA FEDHA HII. Nikaoma ndani nikashangaa sana. Kuna mashirika yanataka kuwasaidia wananchi kuwapa mtaji wa mawazo na fedha waweze kujilimia bustani; kufuga samaki. Watatoa na vifaa vya kumwagilia kwa matone. Watatoa mitambo isiyotumia nguvu za umeme wala mafuta kumwagilia. Wanataka kusaidia watanzania kama elfu mbili.
Cha kushangaza mwandishi hajitaji; hasemi semina hiyo ilifanyika wapi; haainishi msaada huo utatolewa eneo gani la nchi.


Nikajiuliza swali- Hawa wenye gazeti wanajua tunakokwenda? Wanashiriki na kuchangia kwenda huko? Wahaya wana methali moja inasema: if you don’t know where you are going, any way will take you there.

Hivyo lazima wote tufahamu tulipo, tunakotakiwa kwenda na tushiriki kuanza safari kwa pamoja na kwa umoja ili tuweze kufikiamatarajio yetu maana ninatambua hatuwezi kuimba nyimbo mbili tofauti kwa wakati mmoja na sehemu moja

Elisa Muhingo
0767187507

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao