Rouhani amjibu Trump na kusema ni adui wa Iran
Mamlaka za Israel zimemfungulia
mashtaka msichana mpalestina ambaye alirekodiwa kwenye video
akimshambulia mwanajeshi wa Israel.
Ahed Tamimi, 17, na binamu
yake walirekodiwa kwenye video wakiwakabili wanajeshi wa Israel katika
kanda iliyosambaa pakubwa katika mitandao ya kijamii.Anakabiliwa na kesi 12 ikiwemo dhuluma na kurusha mawe.
Lakini familia yake inasema kuwa walihusika kwenye maandamano katika eneo linalokaliwa na Israel la Ukingo wa Magharibi.
- Wapalestina wamuita balozi wao kutoka Marekani
- Mwanajeshi wa Israel miezi 18 jela kwa kumuua Mpalestina
- Jerusalem: Mataifa ya kiarabu yalaani hatua ya Marekani
Video hiyo iyorekodiwa tarehe 15 Disemba ilionyesha kikundi cha wanawake akiwemo Tamini, wakiwapiga wanajeshi wawili wa Israel waliokuwa wamejihami vikali.
Ilisambaa sana katika mitandao na wapalestina wengi wamemsifu Tamini kuwa shujaa kwa kuipinga Israel.
Maoni
Chapisha Maoni