Rouhani amjibu Trump na kusema ni adui wa Iran
Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema
rais wa Marekani ni adui mkuu wa taifa hilo kuanzia utosini hadi kwenye
unyayo. Ameyasema hayo akijibu ujumbe wa rais Trump alioutoa kupitia
ukurasa wake wa twitter.
Katika ujumbe wake rais Trump amesema
kuwa waandamanaji wa Iran wanadai haki yao ambayo wamekuwa wakipigania
kwa miaka mingi kuhusiana na njaa na kukosekana kwa uhuru wao.- Rais wa Iran Hassan Rouhani aikosoa hotuba ya Trump
- Ndugu yake rais wa Iran atupwa korokoroni
- Iran: Tutaunda silaha yoyote kujilinda
Polisi mmoja ameuawa na waandamanaji hao ambao baadhi yao wanajihami kwa bunduki aina ya rifle na hivyo kufanya idadi ya watu 13 kuuawa hadi sasa.
Maoni
Chapisha Maoni