Wanaume wametakiwa kujitokeza kwenye madawati ya jinsia yaliyoko mawilayani kwao ili kupata ushauri na suluhu pindi wanapotendewa vitendo vya kikatili toka kwa wanawake katika familia zaoAnna Tindwa Mkuu wa dawati la Jinsia kibondo
Anna Tindwa, Mkuu wa Dawati la Jinsia Kibondo |
Wanaume wametakiwa kujitokeza kwenye madawati ya jinsia yaliyoko mawilayani kwao ili kupata ushauri na suluhu pindi wanapotendewa vitendo vya kikatili toka kwa wanawake katika familia zao
Akiongea na Blog hii jana Ofisini kwake, Mkuu wa Dawati la Jinsia wilayani Kibondo Mkoani Kigoma Anna Tindwa amesema kuwa wanaume wengi wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya unyanyasaji ikiwemo hata Vipigo lakini wamekuwa wakikaa kimya kwa kuona aibu bila kuripoti matatizo hayo
Tindwa aliongeza kusema kuwa, hali ilivyo hivi sasa bado vipo vitendo vya unyanyasaji kwa wanaoume wanavyotendewa katika Ndoa zao, lakini haviripotiwi hali ambayo pengine usababisha madhala makubwa visipopatiwa ufumbuzi
''kwa mwaka 2017 kuanzia mwezi january hadi desemba ofisi yangu ilipokea kesi za malalamiko ya ukatili wa kijinsia lakini walio wengi ni wanawake wanaolalamika na kati ya wanawake kumi wanafika hapa kutoataarifa za kunyanyaswa na wanaume utakuta wanaume ni wawili au hamna kabisa lakini hali inavyoonyesha wanaume wengi wanafanyiwa ukatili kama kupikwa na mangineyo ila wanaona aibu sisi tuahamasisha waje wakae wasikae na maumivu mioyoni mwao'' alisemaTindwa
Kwa upande wao baadhi ya wanaume ambao ni Joseph Chacha na Herma Myaniko, wilayani kibondo, wamekilikuwepo kwa vitendo hivyo miongoni mwa jami na na wanaume wengi uhofu kuviripoti wakifikiri hawawezi kupata haki kwenye madawati ya jinsia kwa maelezo kuwa ni kwa ajili ya wanawake
Licha ya kudai kutopatikana kwa haki za wanaume, Ayubu Julias na Tamasha Richa wao wanasema zipo baadhi ya familia katika makabila hapa nchini ambazo zina namna ya kuishi japo katika jamii uonekana ni unyanyasaji na kueleza kuwa kinachotakiwa ni kurudisha maadili ya mwenyezi Mungu yanaoonekana kuporoka huku Shabani Ndiigeze akisema haki haziwezi kupatikana kutokana na madawati ya Jinsia kusimamiwa na wanawake peke yao
''Familia zingine inategemea wahusika walivyopanga kuziendesha mwanaume akipigwa anaona ndo mapenzi yanakolea na wakati mwinge mwanaume akifanya kazi za nyumbani ndo kujenga familia japo kulingana na mila zetu jamii nyingine uona kama vile mwanaume huyo ananyanaswa japo vitendo vya ukatili vipo na wanafanyiwa wanaume wengi majumbani wengine hawaendi kuripoti kwa kuwahurumia wake zao na wengine kwa kuona aibu'' alisema Tamasha
Nao wanawake ambaoni Leonia Julias na Dorotea Samweli, kutokana na malalamiko ya wanaume kukataa kuripoti kwenye madawati ya Jinsia mara wanapofanyiwa ukatili na wake zao kama vipigo walisema shida ni mfumo Dume kwani wanaume wamejijengea tabia kuwa mwanamke ndo anatakiwa kupigwa na kulalamika na kuongeza kuwa wanaona aibu kusema kuwa nimepigwa na Mke wangu kikubwa ili kuondoa madhala zaidi wameviomba vyombo husika kutoa elimu kwa makumndi hayo
Maoni
Chapisha Maoni