KIBONDO YAENDELEZA UDHIBITI UGONJWA EBOLA

 


DktSimon Omary  Mratibu huduma za Afya Wilaya ya Kibondo

Fiboreen Siwale Mratibu wa Maralia Wilaya ya Kibondo

Aggrey Magwaza Mkuu wa Wilaya ya Kibondo


Mkuu wa wilaya ya kibondo Mkoani Kigoma, kanali Mstaafu  Agery Magwaza amewaagiza wataalamu wa afya kuendelea kufanya tafiti za kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa maralia kutokana na ugonjwa huo kutodhibitiwa kwa ufasaha na kuendelea kuleta athari kwa jamii

Amebainisha  hayo wakati wa kikao Cha kamati ya afya ya msingi ya Wilaya, walipokua wakijadili namna ya kudhibiti ugonjwa huo ambapo amesema maambukizi ya ugonjwa yamekua yakisababisha madhara kwa jamii kutokana na mbu wannasambaza vimelea hivyo vya  malaria kushidwa kudhibitiwa ipasavyo 

Aidha katika kikao hicho kilijadili namna ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola ndani ya wilaya ya kibondo huku mkuu huyo wa wilaya akwahimiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo ikizingatiwa Wilaya hiyo iko mpakani mwa nchi,  Ili usienee ndani ya wilaya ya kibondo na kuweka maandalizi ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola

Nao baadhi ya wajumbe walioshiriki katika kikao hicho Vedasto Pesambili na Hamisi Tahilo, wameomba elimu zaidi iendelee kutolewa kwa wananchi kuhusiana namna ya kupambana na ugonjwa huo Ili uweze kudhibitiwa

Akiwasilisha taarifa mbele ya kamati hiyo mratibu wa maralia wilaya ya kibondo Fibinoreen siwale amesema wameendelea kuchua hatua mbalimbali za kuudhibiti ugonjwa huo Ili kuweza kuutokomeza ndani ya wilaya ya kibondo

 Kwa upande wake msimamizi wa huduma za afya wilaya ya kibondo dokta Saimoni Omary amesema kama wilaya wamekwisha jipanga vizuri kwaajili ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola ndani ya wilaya Ili kuweza kuakbiliana na ugonjwa huo wakati utakapo tokea

Maoni