UWINDAJI HARAMU WASABABISHA IDADI SOKWE KUPUNGUA GOMBE

 














Na Emmanuel Matinde Kigoma

Idadi ya wanyama aina ya Sokwe katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe iliyoko mkoani Kigoma, inaelezwa kupungua kwa kasi kutokana na kuwindwa, kuharibu maeneo yao ya asili, pamoja na shughuli za kibinadamu ambazo zinahatarisha maisha yao.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Utafiti wa Sokwe kutoka Taasisi ya JANEGOODALL (JGI), Dr. Deus Mjungu, huku akitoa wito kwa wadau wote kuona umuhimu wa kuwalinda Sokwe ili waweze kuongezeka.

 

Nchini Tanzania Sokwe, hupatikana katika mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi lakini kuongezeka kwa idadi ya watu na katika maeneo yaliyo karibu na makazi yao kunatajwa kutishia maisha yao amesema ShedrackKamenya Mhifadhi Mkuu Mstaafu toka Taasisi ya JGI.

  

Ikumbukwe kuwa wanyama aina ya Sokwe ambao tabia zake hufanana kwa asilimia 98% na binadamu, ni kivutio cha utalii kinachoiingizia serikali fedha za kigeni na kusaidia kukuza uchumi hivyo jamii ina jukumu la kushirikiana na serikali kuhakikisha wanaendelea kuishi.

.

 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

KATIKA KUKABILIANA NA MAJANGA YA MOTO SERIKALI IMETOA GARI LENYE MTAMBO WA KUZIMIA MOTO KATIKA WILAYA YA KIBONDO