SIKU YA UJUZI KWA VIJANA
![]() |
| Monica Mwita Mwanafunzi Veta Mwanza |
![]() |
| Voronica Gabriel Mkufunzi Veta Mwanza |
![]() |
| Flaviana Minda Kaimu Mkuu wa Chuo Veta Mwanza |
Yapo naneno ya Wahenga yasemayo,Ushindi ni
Mwenendo, Mwenendo huo ni Kazi, Kazi ni mawazo, mawazo ni kuelewa na imani, na
hivyo kila kitu kinaanzia kwa binadamu.
Kuendana
na maneno hayo,mnamo 2014, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza
tarehe ya Julai 15 iwe siku ya Ujuzi wa Vijana Duniani, kuweka mikakati ya kuwaandaa
vijana kwa ujuzi unaohitajiwa kuwaajiri na kuwawezesha kupata kazi licha ya
kuwawezesha kwa Ujasiriamali.
Siku ya Kimataifa ya Ujuzi kwa Vijana huadhimishwa kila
tarehe 15 Julai. Siku hii ilianzishwa na Umoja wa Mataifa ili kuhamasisha na
kutambua umuhimu wa kuwapa vijana ujuzi na stadi mbalimbali za kazi ili waweze
kujitegemea kimaisha na kuchangia maendeleo.
Lengo kubwa ni kukumbusha jamii na serikali kutoa nafasi
za mafunzo zitakazowawezesha vijana kupata ujuzi unaohitajika katika soko la
ajira, hasa katika ulimwengu wa sasa wa kidijitali. Veta Mwanza ni moja ya
Taasisi inayomilikiwa na Mamlaka za vyuo vya Ufundi Stadi imekuwa ikitoa
maarifa ya Ujuzi Taaluma mbalimbali kama ususi Ushonaji Ufundi Magar, Bomba, Upakaji rangi na nyinginezo
Baadhi ya Wanafunzi wanaopata ujuzi katika chuo hicho
ambao ni Nuru Samweli na Hapnes Modest wamesema maarifa wanayoyapata katika
chuo hicho yamekuwa yakiwafungua kifikra na kubadilisha mitazamo licha ya
kupata ujuzi
Veronika Gabriel ni Mkufunzi katika fani ya ushonaji yeye
anaeleza kuwa mafunzo yanayotolwa katika chuo hicho yanamwezesha Kijana
kushindana katikasoko la ajira
Aidha Wanafunzi wengine wameeleza kuwa Vijana wasiokuwa na taaluma
wanapata Changamoto nyingi katika kuendesha maisha yao ndiyo sababu wao kutafuta ujuzi maarifa wamebainisha Monica
Mwita na Yohana Maguta wanafunzi wanaopata ujuzi wa uunganishaji wa vyumba kwa
uchomeleaji
‘’Kwa kawaida sehemu zote wanahitaji mafundi hivyo bila ujuzi
ajira lazima liwe tatitazo na sasa popote utakapokwenda kuhitaji kupata namna
ya kutumikia Watu lazima uwe na ujuzi si maneo hivyo ujuzi ni lazima kwa kila
mmoja’’ amesema Yohana
Kwa upandewake Kaimu Mkuu
wa Chuo cha Ufundi Veta Mwanza Flaviana
Minda ameeza kuwa wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha wanaitikia wito wa serikali
kuwapatia Vijana ujuzi ambao unawasaidia
kukabiliana na Changamoto za maisha
‘’Mazao yanayotoka katika chuo hiki, ni bora zaidi na yanafaa
katika Sekta husika hivyo Vijana wote wenye uhitaji wa ujuzi wowote kulingana
na kila mmoja anavyojitambua na mahitaji yake yalivyo, wanakaribishwa’’ amesema
Flaviana








Maoni
Chapisha Maoni