MAHUNDI APONGEZA UWAJIBIKAJI KAKONKO ASHAURI WAONGEZE JUHUDI
Na Cosmas Makala
Kakonko
Kakonko. Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Maryprisca Mahundi, amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma, ambapo alianza kwa kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kakonko. Katika kikao hicho, alipatiwa taarifa ya maendeleo ya Wilaya iliyowasilishwa na mkuu wa wilaya Col. Evance Mallasa ikieleza mafanikio yaliyopatikana pamoja na hatua mbalimbali zinazochukuliwa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa manufaa ya wananchi.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Mhe. Mahundi aliupongeza uongozi wa Wilaya ya Kakonko ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya,Col. Mallasa kwa usimamizi mzuri wa shughuli za maendeleo,Pia aliwapongeza Mh. Mbunge Alan Mvano, Katibu Tawala wa Wilaya Maulid Said Mtulia, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Ndaki Stephano Mhuli, kwa ushirikiano na ufanisi wanaouonyesha katika kusimamia utekelezaji wa mipango ya Serikali, jambo ambalo limechangia kuimarika kwa utoaji wa huduma kwa wananchi.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri alipata fursa ya kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ambapo aliwapongeza kwa kujituma na kufanya kazi kwa weledi. Aliwataka kuendelea kudumisha nidhamu, uwajibikaji na mshikamano katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ili kuongeza tija katika utoaji wa huduma za umma na kuendelea kujenga imani ya wananchi kwa Serikali yao.
Mhe. Mahundi alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imejielekeza katika kuwaletea wananchi maendeleo kupitia utoaji bora wa huduma za kijamii na kiuchumi. Hivyo, aliwahimiza watumishi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uzalendo ili kuhakikisha malengo ya Serikali ya kuboresha maisha ya Watanzania yanafikiwa.
Pia aliwashauri kuchangamkia fursa wanazo kutananazo katika maeneo yao ya kazi kama kununua viwanja, mashamba, kujenga nyumba za kuishi na kupangisha ili kujiongezea kipato katika maisha yao ya kila siku na kuacha dhana ya Watoto wanaowazaa kwenye familia kuwaacha kwenye malezi ya Bibi na Babu na badala yake waweze kuwalea wenyewekama familia.

.jpg)






Maoni
Chapisha Maoni