Kibondo;Mkuu wa wilaya ya Kibondo mkoani kigoma Luis Bura amemwagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo kuwasimamisha kazi watumishi 3 wa idara ya ujenzi kutokana na ubadhilifu wa fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba ya walimu katika shule ya sekondari Itaba
Kibondo; Mkuu wa wilaya ya Kibondo mkoani kigoma Luis Bura amemwagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo kuwasimamisha kazi watumishi 3 wa idara ya ujenzi kutokana na ubadhilifu wa fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba ya walimu katika shule ya sekondari Itaba Watumisha hao wanatuhumiwa kudanganya ili mkandarasi anaejenga nyumba hizo kulipwa milion 109 malipo ya wamu ya pili kwa madai kuwa ujenzi umekemilika kwa asilimi 85% ambapo milion 46 zimelipwa bila kufanyiwa kazi yoyote huku ujenzi ukiwa chini ya viwango na ukiwa uko chini ya asilimia 50% kama alivyoeleza mkurugenzi wa halmashauri hiyo Juma Mlehe kwa waandishi wa habari na wananchi Mkuu huyo wa wilaya katika maelezo yake alisesema matatizo ya ubadhilifu wa fedha za serikali katika wilaya hiyo yamekuwa ni mambo ya kawaida huku akilalamikia makundi ya wanasiasa kuingilia shughuli za kitaalam kwa kuwalazimisha watumishi wa halmashauri kufanya mambo wanayoyataka wao na kuwa...