HALMASHAURI YA KAKONKO LICHA YA KUPATA HATI SAFI YATAKIWA KUENDELEA KUREKEBISHA MAPUNGUFU
Kakonko.Licha ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma kupata hati isoyokuwa na mashaka, katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za serikali mwaka 2021/22 imeagizwa kuondoa mapungufu yaliyobainika wakati wa ukaguzi
Thobias Andengenye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma amesema hayo kwenye baraza maalum la kupokea taarifa na mapendekezo ambapo amesema kujibu hoja hizo kutasaidia kuboresha utendaji kazi na kuendelea kupata hati safi na kuwataka kudhibiti hoja badala ya kuwa mabingwa wa kujibu hoja
Amewataka Madiwani kutekeleza na kusimamia Miradi na fedha za serikali katika maeneo yao, na kuwahudumia Wananchi kwa uaminifu ili waweze kuacha alama katika kipindi cha uongozi wao huku akiipongeza halmashauri hiyo kwa utendaji mzuri wa usimamizi wa fedha za serikali
Aidha ameiagiza halmashauri hiyo kuwachukulia hatua Watumishi wote ambao hawataki kufuata sheria na kanuni za kiutumia ambao wamekuwa wakpelekea kuibuka kwa hoja zisizokuwa na msingi
Nzuri Mliduu Katibu tawala Mkoa wa Kigoma amesema hoja nyingi zilizobainika zlitoka katika Idara na Vitengo vya Halmashauri hiyo hivyo wahusika hawana budi kushirikiana kwa pamoja na kupata majibu ya hoja hizo na kuzimaliza pale inapowezekana
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Kakonko Ndaki Mhuri ameahidi kuhakikisha wanajibu hoja zilizobainika kwa kufuata maelekezo yaliyotolewa kwa wakati kwani wameshaanza mikakati ya kuhakikisha hoja hizo zinajibiwa ambapo kulikuwa na hoja za miaka ya nyuma 84 hadi 2023 zimebaki 26
Nao baadhi ya Wananchi waliohudhuria Kikao hicho ambao ni Edson Sehele na Jonathani Kasigala wamepongeza hatua hiyo ya halmashauri kupata hati safi na kuitaka kufuata ushauri wa Mkuu wa Mkoa kulingana na maelekezo ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali
Thobias Andengenye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma alipokuwa akilihutubia Baraza la Madiwani Kakonko |
Maoni
Chapisha Maoni