KAKONKO WAIPONGEZA SERIKALI KUPITIA JWTZ KURUDISHA MWASILIANO YALIYOHARIBIWA NA MAFURIKO
Stephan Ndaki Mkurugenzi Mtendaji Hshauri ya Kakonko |
Gerad Baseke Mkuu wa Shule Ikambi Sekondari |
Kanali Evance Malasa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko alipokuwa akiongea na Wananchi wakati wa uzinduzi wa Daraja jipya lililojengwa baada ya Mvua kuharibu Miundombinu Mto wa Muwazi |
KAKONKO WAIPONGEZA SERIKALI KUPITIA JWTZ KURUDISHA MWASILIANO YALIYOHARIBIWA NA MAFURIKO
Na Muhingo Mwemezi Kakonko
Kakonko Wakazi wa Vijiji vya Kakonko, Itumbiko na Ikambi Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma wameipongeza serikali kupitia Jeshi la Wananchi Tanzania kwa kurudisha mawasiliano ya Barabara yalikatika kutokana na mafuriko yayaliyotokea April Mwaka huu kusababisha wanafunzi kwenda shule na wakulima
Wakiwa kwenye uzinduzi wa Daraja lililojengwa kwa msaada wa JWTZ uliofanyika kwenye kijiji cha Itumbiko wamesema mvua hiyo iliwasababishia hasara kubwa pale waliposhindwa kufika mashambani na kwenda kupata matibabu baada ya barabara kukatika
Wamesema mara maji yalipozuia njia wakulima wengi walikuwa bado hawajatoa mazao ya mashambani Katika eneo la Ikambi hivyo mawasiliano kati ya mji wa Kakoko na Vijiji vingine wananchi walishindwa kuvuka kuvuna mazao na kuwasababishia hasara kubwa lakini kwa sasa waatafanya shugulizao kwa uhakika kwenda kurudi kwani eneo la ikambi ndiyotegemeo kubwa la wakulima wa Kakonko pia huko ndiko iliko shule ya sekondari Ikambi
Gerad Baseke Mkuu wa shule ya sekondari Ikambi anasema Mvua hiyo ilisababisha adha kubwa Wanafunzi kushindwa kwenda shule na kulazimika kuhamishiwa shule nyingine kwa muda hatua ambayo ilipekea Wanafunzi na walimu kuwa katika hali ya usumbufu na kupelekea kutofanya vizuri katika shughuli zao huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kakonko Stephan Ndaki alipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzani kwa kujituma kufanya kazi nzuri za kuwasaidia wananchi katika Majanga
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanal Evance Malasa amesema Wananchi wanatakiwa kutambua thamani ya msaada huo kwa kulinda miundo mbinu ya Daraja hilo isiharibiwe kwani Vyuma vilivyotumika kujenga Daraja hilo ni Garama za serikali na vinatafutwa na Watu kwa ajili ya vyuma chakavu hivyo huenda watu wasitambu umuhimu wake na kusisitiza kutoharibu Miundombinu yake
Maoni
Chapisha Maoni