UKOSEFU WA WATAALAM WA MAZINGIRA VIJIJINI
Kibondo.Ili kuweza kufanikisha mapambano ya mabadiliko ya Tabia nchi serikali imeshauri kuweka utaratibu wa uwepo wataalam wa mazingira katika maeneo ya vijijini kama ilivyo kwa maafisa ugani ili watoe ushauri wa utunzaji wa mazingira
Hayo yalisemwa jana na baadhi ya Wakazi wa Wilaya za Kakonko na Kibondo Mkoani Kigoma ambao ni George Daniel na Joyce Alex walipokuwa kwenye mafunzo ya utunzaji wa Mazingira yaliyoandaliwa na Kanisa la Free Pentekoste Jimbo la Kibondo ambapo wamesema Wananchi wengi wanaoishi Vijijini wanashindwa kuendesha shuguli za upandaji Miti kutokana na kukosa uelewa
Wamesema kwa sasa kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa Wananchi katika sualautunzaji wa mazingira hasa katika upandaji Miti lakini wamekuwa wakikosa uelewa na kuharibikiwa katika Vitaru ya uoteshaji na Mashambani hatua ambayo imekuwa ikipekea hali ya kukata tamaa
''Tunawaomba Wadau wa Mazingira na serikali kulitazama kwa umakini suala hili kwani miti imekuwa ikikatwa hovyo hivyo jitiada za upandaji wakitaalam ni wa lazima pamoja na hamasa ili kufikia malengo yanayokusudiwa''alisema George Mshiriki wa mafunzo
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Mazingira kupitia Jimbo hilo Leopod Muhagaze amesema katika kuhakikisha wanatimiza malengo yao upandaji Miti, wamekuwa wakishirikiana na maafisa Mazingira ngazi za wilaya Kakonko na Kibondo kuyaelemisha Makundi katika maeneo ya Vijijini japo hawakidhi haja
Katika hatua ya kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa Wataalam wa Mazingira kwenye kata na Vijiji upo mpango wa kutoa elimu kwa Viongozi wa Vikundi ambao nao watawaelimisha wenzao Vijijini namna ya upandaji Miti ulinzi wa vyanzo vya Maji pamoja na sheria na sera za utunzaji wa Mazingira
Aidha Leopod aliongeza kuwa licha ya Vikundi kuhamasihwa kutunza Mazingira wamekuwa wakipewa elimu ya kuinua uchumi wao kupitia Vikundi vya ujasriamali ambapo Wananchi wamekuwa wakipewa Mbegu na Vifaa vya kumwagilia Miche
Kanisa la FPCT Jimbo la Kibondo liliamua kuanzisha mradi wa Mazingi kwa waumini wake ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamekuwa yakipelekea kushuka uchumi lina lenga kuhumia Vikundi 100 na hadi sasa vipo vikundi 50 11 viko wilayani Kibondo na 39 viko wilaya ya Kakono na zimeshatumika Sh 17 milion kuanzi januari 2022 hadi sasa
Mpango huo ulifanikisha kupanda Miti elfu kumi kwa mwaka 2022 kupitia Vikundi na Mtu mmoja mmoja katika maeneo ya Makazi kama anavyoeleza Askofu wa Kanisa Hilo Jimbo la Kibondo Enos Ntibalosiga huku akisistiza waumini wa Kanisa hilo kutambua umuhimu wa utunzaji wa Mazingira
Washiriki wakiwa kwenye Mafunzo ya utunzaji wa Mazingira |
Leopod Muhagaze Mratibu Mradi wa Mazingira na Mkufunzi |
george Daniel Mshiriki |
Enos Ntibalosiga Askofu Kanisa FPCT Jimbo la Kibondo |
Maoni
Chapisha Maoni