KANEMBWA JKT WAZINDUA MRADI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

 






Muhingo Mwemezi Kanembwa

Licha ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT kutoa mafunzo ya ulinzi kwa Vijana linayo mikakati ya kuendeleza Kilimo cha mazao ya Chakula na Biashara  kama Mahindi Maharage,Alizeti, Mpunga na mengineyo kupitia Idara zake husikandani ya Jeshi hilo

Peter Lushika Mkurugenzi Kilimo Mifugo na Uvuzi Jeshila kujenga Taifa akiwa katika hafla ya uzinduzi wa Kilimo cha umwagiliaji mpango unaoshirikisha Shirika la Kilimo Duniani FAO, iliyofanyika katika Kikosi cha 824 Kanembwa Jkt Kakonko Mkoani Kigoma ameeleza Mikakati ya Kilimo katika Jeshi hilo kuwa ni kulima Mazao ya Chakula na Biashara  kama Mahindi,Alizeti,Maharage na Mpunga

Amesema  kulingana na serikali kujielekeza katika Mazao ya Kimkakati kama Michikichi na Alizeti, Jeshi hilo linao mpango maalum wa kuendesha Kilimo cha mazo hayo na mengineyo na licha ya kuwepo kwa changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi, wamejianadaa vema kwa kuanzisha kilimo cha umwagiliaji  ili kilimo kiendelee nyakati zote

Kwa upande wake Kaimu Kamanda Kikosi 824 kj Meja Benito Lubida,amesema Mradi wa umwagiliaji katika Kikosi hicho, ulioanzishwa kwa kushirikiana na Shirikala Kilimo na Chakula ulimwenguni FAO  unathamani ya Shilingi za Kitanzania 110 Milion na mbegu zinazozalishwa kikosini humo kama Maharage na Viazilishe wamekuwa wakigawiwa Wananchi Wilaya za Kakonko Kibondo na Buhigwe  na kuwapa mafunzo katika Mashamdarasa, 

 Nae  mwakilishi wa Shirika la Kilimo na Chakula Duniani FAO Nyabeni Tito ameahidi   kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuwasaidia Vijana kupitia mpango wa pamoja Mkoani Kigoma huku akipongeza Kikosi cha 824 KJ Kanambwa JKT kwa kufanya kufanya vizuri katika ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji ambayo itasadia kuleta tija katika kilimo

Baadhi ya Vijana waliobahatika kujiunga na Mafunzo ya Kijeshi Kikosini hapo wamepongeza hatua mbalimbali zinazofanyika kuwapatia stadi za Maisha ambapo wamesema wengi wao walianza mafunzo wakiwa hawawezi kufanya kazi lakini hadi wanahitimu mafunzo wameweza kubadilika na hata watakapomaliza muda watasaidika kwa kufanya kazi kiongezea Vipato na kuendesha maisha yao hasa katika masuala ya Kilimo

Kaimu Kamanda Kikosi 824 kj Meja Benito Lubida







mwakilishi wa Shirika la Kilimo na Chakula Duniani FAO Nyabeni Tito

Kanali Peter Lushika Mkurugenzi wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Jkt 




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji