Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma,Baadhi ya Wawakilishi wa Masirika wakiwa kwenye Kikao cha pamoja yatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na serikali
Baadhi ya Wawakilishi wa Mashirika wakiwa kwenye Kikao cha pamoja kilichofanyika Ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kibondo |
Kanali Agrey Magwaza Mkuu wa Wilaya ya Kibondo aliyekuwa mwenyekiti Kikao cha pamoja Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali |
Kibondo.Mashirika yanatoa hudumablimbali za Kijamii yametakiwa kufanyakazi kwa ushirikiano na kufuata taratibu ndipo malengo yatakapofikiwa
Agrey Magwaza ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo amesema hayo kwenye Kikao cha Baraza la Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali kilichofanyika Mjini Kibondo kwa lengo la kufanya tathmini ya utendaji wao wa kazi, Mbapo ameeleza kuwa wakiwa na ushirikiana ndipo watakapokuwa na utendaji wenye tija
Magwaza ameongeza kuwa iwapo watashirikiana pamoja watapata fursa ya kupashana habari na utaratibu huo utasaidia kupunguza miingiliano ya kiutendaji ambapo ameyataka Mashirika hayo kuhakikisha yanafuata taratibu na sheria zilozpo chini ya muamvuli wa Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya
Baraza hilo linayahusisha Mashirika ya Kimataifa na ya ndani ambapo yamekuwa yakitoa huduma kwa Wakimbizi na kwenye jamii ya Kitanzania ambapo wamejadiliana na kuweka Mikakati ya kiutendaji kwa kuhakiha kila shirika linapotaka kutoa huduma kwenye jamii za Kitanzania lazima lipate kibali maalum na kutoa ushirikiano serikalini kwa kuwahusisha
Wataalam kulingana na hudumaitakayokuwa inatolewa
Mashirika hayo yamekuwa yakifanya kazi kwa kushirikiana na serikali kupitia Idara ya maendeleo ya jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na kuwataka walezi ambaye ni serikali kutambua kazi za kila shirika huku Mwenyekiti wa Baraza hilo Leopod Muhagaze akisema fedha zilizotolewa na mashirika hayo ni 9.5 Bilion ambapo 8.4 zilihudumia wakimbizi na 1.1 Bilioni zilihudumia Miradi Kwa Watanzania mwaka 2022
Mashirika hayo yapatayo ishilini na moja yamekuwa yakitoa huduma kwenye jamii zinazozunguka Mambi ya Wakimbizi na kwingineko katika jumla ya kata 16 kati ya Kata 19 zinazounda Wilaya ya Kibondo na Miradi ambayo imekuwa ikiendeshwa na mashirika hayo ni huduma za Elimu, Afya, kupinga ukatili Maji na utunzaji wa Mazingira
Mwis
Mwis
Maoni
Chapisha Maoni