WOGA KUTOA TAARIFA NA UMASIKINI SABABU KUSHAMILI UKATILI NA MIMBA ZA UTOTONI

 


George Leo Mwakilishi Shirika la World Vision








Kanali Evance Malasa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko aliyekuwa mgeni rasmi maadhimisho siku ya Mtoto wa Afrika



                                      Na Muhingo Mwemezi Kakonko

 

Uelewa mdogo na woga katika jamii hasa Wananchi  wanaoishi Vijijini ni baadhi ya sababu zinazopelekea kushamili kwa Vitendo vya ukatili kwa Watoto kama kuolewa na kupata Mimba za utotoni

Monica Elias na Ruth James ni Wakazi wa Kata ya Katanga wilaya ya Kakonko  Mkoani Kigoma wamebainisha kuwa wananchi wengi wanaoishi Vijijini wamekuwa wakiingiwa na woga kutoa taarifa kwenye vyombo vya Dora baada ya Watoto  wakufanyiwa Vitendo vya ukatili wakihofia kupata madhala kutoka kwa waharifu

Wamesema kuwa mara nyingi wanaofanya vitendo vya ukatili utumia fedha kujihami hivyo hata wenye watoto ambao ni wahanga wa ukatili kama kupata za  Mimba za utotoni  ushindwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya Dora ambapo wameongeza kuwa hata umasikini wa kipato katika baadhi ya familia ni changamoto kwani watoto  wengi uacha masomo na kwenda kufanya kazi za kujiongezea vipato ikiwa ni pamoja na baadhi ya Wazazi na walezi kuwa na tama za mali na kuitaka serikali kuendelea kutoa elimu kwa Wananchi ili wajitambue na kudai haki zao kwa mujibu wa taratibu na sheria

Nao baadhi ya Watoto ambao ni Tamari Amosi na Edgar Bakera wamewaomba wazazi kutimiza wajibu wao kwa kuwalea wao na kuwapatia mahitaji yao ya msingi licha ya changamoto zilizopo huku baadhi ya Wadau wakiomba serikali kutoa ushawishi wa mabadiliko ya sheria zinazotoa idhini ya   mahakama  na wazazi kuwaozesha watoto katika umri ambao haukubariki  kiafya  alisema mwakilishi wa shirika la World Vision  George Leo

;;Kwakuwa Watoto wengi wanakuwa hawajakomaa kimwili na kiakili, hivyo mara  wanapokumbana na changamoto ya kuolewa kabla ya wakati hali hiyo inapelekea kusababisha madhala makubwa  hivyo ni vema zikafanyika jitiada za makusudi ili kunusulu makundi ya Watoto; alisema George

Akiwa Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto waafrika  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Evance Malasa  yeye anawataka wazazi  na walezi kushikiana kwa pamoja kutoa taarifa kwenye vyombo vya Dora mara wanapoona vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa Watoto ili hatua zichukuliwe

Jamii haina budi kulivalia njuga suala la ulinzi wa Watoto kwani serikali ipo wala hakuna haja ya kuogopa kudai haki suala la msingi ushaidi wa kweli uwepo linapotokea jambo kila Mwananchi ana haki ya kusikilizwa hi Mtu yeyo anaweza kutoa taari kwa mwenyekiti wa kitongoji,Kijiji au Mtaa au kwa kiongozi yeyote wa Dini hata kama ni kwa ngazi ya familia pia wapo Polisi kwenye kata na watendaji wa kata na Vijiji wote wapo kwa kwaajili ya kutatua kushauri pale wananchi wanapopata changamoto

Adha Malasa amewataka Wazazi,Walezi na Jamii kwa ujumla kuacha kukaa kimya na kuhakikisha wanatoa malezi bora kwa Watoto wao na kuacha kuwatumia kwenye biashara hasa kwenye masoko ya usiku katika maeneo ya Vijijini ili kuepusha kukumbwa na vishawishi vinavyopelekea kukatisha Ndoto zao

Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika 2023  yamefanyika kiwilaya katika Kijiji cha Katanga Kata ya Katanga Wilayani Kakonko kwa kushirikisha Mashirika mbalimbali yasiyoya kiserikali na Halmashauri ya Wilaya huku mdhamini Mkuu akiwa ni shirika la World vision

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji