RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI SGR NA KUZINDUA MELI NNE ZA MIZIGO ZIWA TANGANYIKA
![]() |
| Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania |
![]() |
| Alan Mvano Mbunge Jimbo la Kakonko |
![]() |
| Simon Siro Mkuu wa Mkoa wa Kigoma |
![]() |
| Makame Mbalawa Waziri wa Uchukuzi |
Na Emmanueli Matinde,Kigoma
Kigoma.Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amwesema serikali
imeendelea na jitihada mbali mbali za kuimarisha miundombiu ya usafiri na
usafirishaji nchini ikiwemo ujenzi wa Reli ya kisasa, uendelezaji wa bandari na
ujenzi wa barabara na viwanja vya ndege.
Dkt. Samia amesema hayo leo mkoani Kigoma mara
baada ya kuzindua meli nne za mizigo ndani ya Ziwa Tanganyika, na kuweka jiwe
la msingi la ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) Tabora – Kigoma, chenye urefu wa
kilomita 506 kitakachojengwa kwa gharama ya Shilingi Trilioni 7.4.
Amesema yote hayo yanafanyika kwa lengo la
kuifungua nchi kibiashara na kiuwekezaji, kupunguza gharama za usafiri na
usafirishaji na kurahisisha biadhaa kuyafikia masoko ya ndani na ya nje ya
nchi.
Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame
Mbarawa, amesema meli nne mpya zilizozinduliwa, zitafungua enzi mpya za
usafirishaji wa majini katika Ziwa Tanganyika, zitaongeza wa usafirishaji wa
mizigo, kuimarisha usalama wa safari, kupunguza gharama za usafirishaji na
kuimarisha biashara kati ya Tanzania, Congo na Burundi.
Wakizungumza kwa niaba ya wananchi Mbunge wa Jimbo
la Kigoma Kusini Nuru Kashakali, na Mbunge wa Jimbo la Kakonko Alan Mvano,
wamesema Reli ya SGR inakwenda kupanua wigo wa biashara baina ya watu wa mkoa
wa Kigoma na wa nchi jirani za Burundi na Congo DRC.
‘’Kwakweli tunaishukuru
Serikali kwa jitiada zake zakuhakikisha Mkoa wa Kigoma na maeneo mengine
yanafunguka kwani imekuwa ni vigumu wafanyabiashara kufikia mafanikio kutokana
na garama kubwa za usafirishaji wa bidha kati ya Congo Kinshasa na Burundi kwani
yanayotumika ni Magari pekee ila usafiri wa Meli na Reli utakuwa mkombozi’’
amesema Mvano







Maoni
Chapisha Maoni