BOSI TRA MIAKA 20 JERA

 Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma imemhukumu kifungo cha miaka ishirini gerezani aliyekuwa Meneja wa TRA Wilaya ya Kibondo, Irving Bagasheki, baada ya kupatikana na hatia katika makosa mawili ya kujihusisha na nyara za serikali kinyume cha sheria.

Hukumu hiyo imetolewa Juni 29, 2026 na Hakimu Mkazi Mfawidhi Aristida Tarimo mbele ya jopo la mawakili wa serikali, baada ya ushahidi wa upande wa mashtaka kuthibitisha bila kuacha shaka kwamba Bagasheki alihusika na usafirishaji wa meno ya tembo mawili yenye thamani ya shilingi milioni 52.

Mnamo Julai 1, 2024 Bagasheki alikamatwa katika eneo la Kihomoka wilayani Kakonko mkoani Kigoma akiwa ndani ya gari ya serikali lenye namba za usajili STL – 7274 akijaribu kusafirisha meno ya tembo kinyume na sheria za nchi, Baada ya kukamatwa Bagasheki na wenzake watano walifunguliwa kesi namba 4733 ya mwaka 2025 kwa makosa ya kupatikana na nyara za serikali isivyo halali.

Katika kosa la kwanza, mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha miaka ishirini, jela na katika kosa la pili pia amehukumiwa kifungo cha miaka ishirini jela, lakini kwa kuwa makosa yote yanaenda sambamba, mahakama imeamuru atatumikia kifungo cha miaka ishirini pekee.

Hata hivyo, washitakiwa wengine watano ambao ni Hosea Bwandu Ntakimulela, Mathias Kimanuka, Daniel Ezekiel Mbwambo, Ngendamenya Kagozi na Majid Husein Bidebe wameachiliwa huru baada ya mahakama kubaini kuwa hawakuhusiana na makosa hayo.

 


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

KUHITIMISHA UCHUKUAJI FOMU KINYANG'ANYIRO CHA UBUNGE JIMBOLA MUHAMBWE CCM