Mkapa aongoza mazishi ya Meja Jenerali Lupogo
Rais mstaafu akiweka shada la mauwa kwenye kaburi la meja Gerali msitafu Herman Lupojo wakati wa Mazishi RAIS mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa jana aliwaongoza viongozi mbalimbali na mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Meja Jenerali mstaafu Herman Lupogo kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange pamoja na Jenerali Mstaafu Robert Mboma. Akisoma risala mara baada ya mazishi, Mwakilishi wa JWTZ, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, alisema marehemu alifariki dunia Oktoba 19 mwaka huu kwa ugonjwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo alikokuwa akipata matibabu. Alisema, marehemu alimaliza elimu ya Kidato cha sita katika shule ya Sekondari Pugu mwaka 1956, baadaye akapata Stashahada ya Ualimu na Shahada ya kwanza ya Sanaa katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda. “Marehemu alijiunga na Jeshi ...