Serikali yafunga migodi ya machimbo ya Dhahabu
Issa Machibya mkuu wa mkoa wa kigoma alipokuwa akiongea na wananchi wa kijiji cha kinyinya wilayani kakonko alipotoa amri ya kufunga migodi ya dhaabu |
Wananchi wa kijiji cha kinyinya wakiwa mkutanoni |
Kamati ya ulinzi usalama kigoma wakiwa ktk mkutano wa hadhara katika kijiji cha kinyinya kwa ajili ya kuona namna ya kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji |
abu
Serikali imeamulu kufungwa kwa migodi yote ya machimbo ya Dhaabu
iliyoko katika kata ya Nyamtukuza wilaya
ya Kakonko Mkoani Kigoma
Amri imetolewa na mkuu wa mkoa
huo Issa Machibya alipokuwa akiongea na wananchi wa Kijiji cha Kinyinya
wilayani humo kwenye mkutano wa hadhara alipokwenda kujionea hali halisi ilivyo
baada ya kutokea mapigano ya wakulima wakigombea ardhi hatua iliyopelekea jumla
ya watu watatu kupoteza maisha katika maeneo ya mashambani
Uamzi huo umekuja baada ya wakazi wa wakijiji hicho kutoa maelezo yao kuwa chanzo cha vulugu
ni ni migodi hisiyokuwa rasmi inayokusanya watu kutoka sehemu mbalimbali ambapo
watu wengi waliingi katika vijiji vya Tarafa hiyo na baadae wageni hao kuamua
kujichukulia ardhi na kuingiza mifugo bila utaratibu na sheria. na baadae
kusababisha vitendo vya ujambazi na kugombania ardhi
Aidha wakazi hao wameomba serikali kushugulikia matatizo hayo,
ikizingatiwa wakati huu ni msimu wa kilimo, kwani hivi sasa hawawezi kwenda
mashambani kuendelea na kazi zao za kilimo kwa kuhofia kuvamiwa na waakulima
wenzao na kufanyiwa vitendo vya kikatili kupigwa viboko na kujeruhiwa kunyang’nywa mali zao
Wamesema kuwa wapo baadhi ya jamaa zao ambahawajulikani walipo baada ya
kuanza kuvamiwa na watu waliowataja kuwa ni wasukuma na kufanyiwa vurugu
Pamoja na mambo mengine wakazi hao wameendelea kuushutumu uongozi wa
kijiji hicho kwa kutofuata taratibu na sheria kwa kuwakaribisha wageni bila
kuwashirikisha wananchi katika mikutano ya kijiji bali wao uenda kukusanya hela
kwa wakulima na wafugaji wanaohamia katika kijiji hicho hali inayoleta usumbufu kwa wenyeji kwa
kuchukulia ardhi zao na kulishiwa mifugo kwenye mashamba yao ambapo
wanapopeleka malalamiko katika uongozi wa kijiji hayafanyiwi kazi
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha kinyinya Justin Kilegea
alikanusha tuhuma zilzoelekezwa kwake na kusema hela zilizowahi kuchangishwa
kwa wakulima wahamiaji ni zilikuwa kwa ajili ya kuendeleza benki ya Matofari ya
kijiji, ila mgogoro ulitokea baada ya ya mfugaji kuuwa na ng’ombe wake
kukatwakatwa na watu wasiyojulikana
Mkuu wa mkoa huo alitoa wito
kuwa watanzania wote wanatakiwa kuthaminiana kwakuwa katika nchi hii hakuna
mambo ya kikabila na kila mtu ana haki ya kuishi maali popote bali afuate
taratibu na sheria na kuutaka uongozi wa kijiji na kata hiyo kuhamasisha amani
katika jamii
Machibya alitoa amri ya kufunga migodi yote ya dhaabu Kanyomvi,
Nyamwilonge Lutela na mingine ilioanza
zamani naya karibuni ili utaratibu unaokubalika uweze kufanyika na watu woe
waishi kwa Amani
Wahamiaji hao wanatajwa kuwa waliingia katika maeneo hayo kwa kufuata
madini na ufugaji kasha baadae kuchukua ardhi na kuanza kulima hali
iliyopelekea ugomvi wa ardhi
Hatua hiyo imekuja baada ya mfugaji mmoja kuuwawa na watu
wasiyojulikana na Ng’ombe wake kutwakatwa na mapanga na baadhi ya wakulima na
wafugaji wanaotajwa kutoka katika mikoa ya Mwanza na shinyanga kuamua klipiza
kisasi na kuwauwa wakulima wenyeji wawili na wengine kadhaa kupotea.
Maoni
Chapisha Maoni