DED Uyui apewa siku 60

WAZIRI Mkuu,Bw.Mizengo Pinda,amempa miezi miwili (siku60),Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, mkoa ni Tabora(DED),Bi,Khadija Makuani,kuhakikisha watumishi wote wilayani humo wawe wamehamia Isikizya yalipo Makao Makuu ya Wilaya hiyo..

Bw.Pinda alitoa agizo hilo juzi wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Isikizya waliofika kushuhudia uzinduzi wa Makao Makuu ya Polisi wilayani humo. "DED nimekagua nyumba ya Mkuu wa Wilaya na kuzindua nyumba nane,miundombinu iliyopo inatosha,hamia we na watu wako,nataka ifikapo Desemba 31 mwaka huu,wote muwe Isikizya na ambaye atagoma,RC(Mkuu wa Mkoa), niletee jina lake.

"Shauku ya wananchi kuwasubiri mhamie hapa imetosha,mtumishi ambaye atagoma niishara kuwa hataki kuwahudumia wananchi nasisitutasema hatukutaki...watumishi wengi wanajifanya wakubwamno kuliko wananchi mnaowahudumia," alisema Bw. Pinda.

Bw. Pinda aliwasili Mjini Tabora juzi jioni nakutembelea Makao Makuu ya Wilaya hiyo ili kukagua mradi wa ujenzi wa makazi ya watumishi na kuzindua nyumba na zilizojengwa kwa gharama ya sh .milioni 555 ambazo kati ya hizo,sh.milioni 400 ni ruzuku kutoka serikalini.

Pia Bw. Pinda alikagua nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui ambayo iko katika hatua za mwisho za ujenzi na baada alizungumza na wananchi.

Jengo lingine ambalo alikagua ujenzi wake ni Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ambayo ni ghorofa moja ambalo awamu yakwanza ya ujenzi itagharimu sh.bilioni 1 .1 na a wamu ya pili sh.bilioni1.4.

" Wakati tukisubiri ujenzi wa ofisi hii  ukamilike,tafuteni nafasi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili muweze kuwakaribu na wananchi na kutatua changamoto walizonazo,"alisema.

"Mnakaa Tabora Mjini halafu mnadai mnawatumikia wananchi wa Uyui jambo ambalo haliwezekani,hayo mafuta mnayotumia kwenda na kurudi mjini mngetembelea wananchi wa vijijini na kuhimiza shughuli zamaendeleo," alisema.

Bw.Pinda alisisitiza kuwa;"Kama mngehamia mapema,tatizo la maji lingekuwa limetatuliwa na ujenzi wanyumba za watumishi wote ungeshakamilika," aliongeza.

Akizungumzia changamoto ya uhabawamaji, Bw.Pinda aliahidi kuwatafutia sh.milioni200 kutoka Wizara husika ili ziwezeshe kuvuta maji kutoka chanzo cha Igombe kilichopo kilomita 35 kutoka Isikizya.

Aliwapongeza askari walioamua kuhamia Isikizya licha ya mazingira magumu waliyoyakuta akisema atawasiliana na Mkuuwa Jeshi la Polis inchini(IGP)iliwaone na mbaya kuwasaidia wapate nyumba pacha mbili au tatu ambazo zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa(NH C).

Alimtaka Mkuu wa Mkoa huo, Bi.Fatma Mwassa, aangalie uwezekano wa kuwatumia vijana waliojiunga na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT)ili kupata utaalamu wao na kuu hamishia kwa wananchi.

"RC tafuteni na yakutumia utaalamu wa vijana wa JKT ili wawafundishe wananchi mbinu za kilimo bora ,ufugaji bora au ujenzi wa nyumba bora, msiwatumie kwa kuimba tu," alisema

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji