Nec yaanza kuboresha Daftari la Wapigakura
Makamu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi NEC hamid Mahamudu akizungumza na Waandishi wa Habari kulia ni mkurugenzi wa uboreshaji wa Daftari la wapiga kura Julias Malapa |
Nec imebainisha hayo
jijini Dar es Salaam jana ikieleza kuwa tayari Serikali imetoa Sh15
bilioni za uboreshaji huo na kwamba utakamilika Serikali itakamilisha
kutoa Sh270 bilioni zinazohitajika kwa ajili ya uboreshaji wa daftari
hilo.
Hadi sasa, kuna mkanganyiko kuhusu tarehe hiyo
baada ya Rais Jakaya Kikwete kutaja mwezi Aprili mwakani kama wakati wa
kupiga kura hiyo, akipingana na Machi 15 iliyotolewa na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema.
Makamu
mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid, alisema jijini Dar
es Salaam jana kuwa tume hiyo itakamilisha daftari hilo ifikapo Aprili
mwakani.
‘’Mpaka sasa Serikali imeshatoa Sh15
bilioni, tutaendelea kupokea kidogo kidogo kutoka Hazina. Ikiwa zikifika
kwa wakati, tutakamilisha zoezi hili Aprili 18 mwakani,’’ alisema na
kuongeza: ‘’Mtakumbuka awali tuliarifu wananchi kuwa zoezi la uboreshaji
wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura lingeanza Septemba mwaka huu, hata
hivyo halikuanza kutokana na kuchelewa kupatikana kwa fedha kutoka
serikalini.’’
Alisema kuwa kwa sasa Nec imeanza kupewa fedha na Serikali kuwawezesha kuanza kwa zoezi hilo la uboreshaji daftari hilo.
Jaji
Hamid aliongeza kwamba mara baada kupokea kiasi hicho pamoja na vifaa
vya uboreshaji wa daftari hilo, Nec ilianza kutoa mafunzo kwa watendaji
wake.
“Novemba mwaka huu, tutafanya majaribio ya
uboreshaji daftari la wapigakura kutumia mfumo wa ‘Biometric Voter
Registration’ katika majimbo matatu ya uchaguzi ya Kawe Manispaa ya
Kinondoni, Halmashauri ya Mji wa Kilombero na Mlele Halmashauri ya Mji
wa Katavi,” alisema.
Maoni
Chapisha Maoni