Watu wawili wafa katika mapigano kugombania ardhi na ukabila
Wananchi wa kijiji cha Kinyinya wakimsikiliza Dc |
Askali Polis wilaya ya Kakonko waliokuwa wanalinda usalama wakati wa mapigano kati ya wakulima Waha na Wasukuma Kijiji cha kinyinya na Kakonko ambapo watu waili walipoteza maisha |
Venance Mwamoto kaimu mkuu wa wilaya ya kakonkoalopokuwaakizungumza na wakazi wa kijiji cha kinyinya Tarafa ya Nyaronga Kakonko wakati wa vurugu za kugombea ardhi kati ya wasukuma na waha |
Watu wawili wafa katika mapigano kugombania ardhi na
ukabila
Nyumba ya mkulima kijiji cha Kinyinya kakonko |
Watu wawili wamekufa na
wengine hawajulikani walipo baada ya kuzuka mapigano kwa ajili ya kugombania
ardhi kati ya kabila la Wasukuma na Waha
katika kijiji cha kinyinya kata
ya nyamtukuza wilaya ya Kakonko mkoa wa Kigoma
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw Justini Kilegea,
amesema kuwa mapigano hayo yamewahusisha
watu wa kabila la Wasukuma dhidi ya kabila la Waha usiku wa kuamkia jana baada watu wa kabila
la wasukuma wanaoishi mashambani kuvamia nyumba za waha na kuawapiga kwa madai kuwa wanatakiwa
wa waambie majambazi wanaishi wapi
nakuanza kuzusha vurugu kwa kuchoma nyumba na kuuwa watu wawili na wengine
hajulikani walipo
Hata hivyo amedai kuwa
mapigano hayo yamehusishwa na swala la
ulipzaji kisasa baada ya tar 15oktoba 2014 watu wasiyojulikana kumuua mtu mmoja
wa kabila la wasukuma na kutakata Ng’ombe
wake kwenye maeneo hayo ya mashambani ndipo nao wasukuma walipoamua
kulipiza kisasi kwa kuwavamia Waha na kusababisha mauwaji ya waliouwa ni
Kachila Kahegele umri miaka 48 na Lamecki Kachila miaka 26 wate wanaume.
Nae Kaimu mkuu wa wilaya
hiyo Venance Mwamoto na kamati ya ulinzi usalama walifika katika kijiji hicho
na kuwataka wananchi kuacha kushambuliana na kulipiza visasi kwani hali hiyo ni
hatari sana
kwani inaweza kuleta vurugu zisizoisha, baada ya kusikia kuwa Watu wa kabila la
waha nao wameamua kwenda katika maeneo hayo kwa ajili ya kulipiza kisasi juu ya
ndugu zao waliokufa na wengine kupotea
Aidha Mwamoto amewata
wanasiasa kutoliingilia swala hilo kisisa kwani wote wanatakiwa kushirikiana kuweza
kutatua matatizo yao
ili jamii iishi kwa Amani na utulivu
Amesema kuwa kila mtu
anaruhusiwa kuishi maali popote hapa nchini isipokuwa anapotaka kwendakuishi katika
kijiji chochote lazima auone uongozi husika na wananchi washirikishwe kwa njia
ya mikutano ya hadhara juu ya mtu anayeingia katika eneo lao
Kwa upande wao baadhi ya
wakazi wa kijiji hicho, wamesema kuwa mgogoro huo ni wa siku nyingi kati ya
wasukuma na waha wanaoishi mashambani wakigombania ardhi
Aidha wakazi hao
wameulalamikia uongozi wa kijiji hicho kwa kulifumbia macho swala hilo hadi kufikia hatua hiyo kwani wamekuwa wakiwaeleza
mara kwa mara maana wapo baadhi ya watu kama wafugaji wamekuwa wakiingia katika kijiji hicho na kuchukua ardhi nguvu bila utaratibu
Wamesema kuwa wageni wengi
hususa ni wafugaji wamekuwa wakimilikishwa maeneo bila kuwa shirikisha wananchi
hali ambayo imekuwa ikisababisha mvutano mkubwa kati yao na wageni hao
Mwenyekiti wa kijiji hicho
alipoulizwa juu ya tuhuma zinazo mkabili yeye na wenzake kuwa wao ndiyo
wanosababisha mgogoro huo kuwa mkubwa kwa kuufubia macho kwa kugawa ardhi ya
kijiji bila utaratibu na sheria kwa kutowashirikisha
wananchi katika mikutano ya kijiji alikana tuhuma hizo na kudai kuwa yeye
alipoingia madarakani aliwakuta hivyo hajui waliingiaje hapo kijijini na
wanajitahitadi kulishugulikia swala hilo ili aman iwepo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni