DC MAGU AZITAKA MAMLAKA ZINAZOZOJIHUSISHA NA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA KUFANYA KAZI KABLA YA MVUA KUNYESHA

 

Katika kukabiliana na Matatizo ya Mvua kubwa ziilizotabiriwa na Mamlaka ya hali ya Hewa nchini TMA , Mkuu wa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza Jubileti Lauwo,amezitaka Mamlaka zote zinazohusika  kukabiliana na majanga kufanya utekelezaji kazi husika  kwa wakati kabla Mvua hizo hazijaanza kunyesha

Akiongea mara baada ya Kikao na Viongozi  kuanzia ngazi za Vijiji na Wataalam mbalimbali amesema ameziagiza Mamlaka zinazohusika na Miundo mbinu ya Barabara yaani Wakala wa huduma za Barabara za Mijini Vijijini TARURA na TANROAD kuboresha miundombinu hiyo haraka kwani ni muhimu kwa Maisha ya Watu

Aidha amesistiza mikataba inayotajwa kuhakisha inafanyiwa kazi maana Mvua zinatarajiwa kunyesha siku si nyingi zijazo kwa hiyo ni vema Barabara zote zikawa zimeimarishwa mapema na kurekebisha njia za Maji



Jubileti Lauwo Mkuu wa Wilaya ya Magu akiwa kwenye Kikao na Viongozi Wilayani Magu wakijadili namna kuchukua tahadhari ya Elinino

Hata hivyo Jubileti amesema katikaWilaya yakewamejipanga kuhakikisha hayatokei Majanga iwapo kama Mvua zitanyesha nabado wanaendelea kuwaelimisha Wananchi kuhusu Mvua za Elinino

Baadhi ya washiriki wa Kikao hicho , wakatoa ushauri wao juu ya kuimarisha Barabara kwa TANROAD NA TARURA huku Mwakilishi wa TANROAD Mkoa wa Mwanza Ramadhani Majaliwa akieleza kuwa wameshaanza utekelezaji kuhakikisha Barabara zinapitika muda wote

Kwa kuwa Mvua hizo zinatarajiwa huenda zikaanza kunyesha mwishoni mwa mwezi Septemba au mwanzo ni mwa Oktoba, ushauri ukatolewa juu ya suala la utoaji taarifa za haraka iwapo linatokea jambo kwa ajili ya msaada wa haraka ameeleza Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Magu Mohamed Kyando


Kwa kuwa Mvua hizo zinatarajiwa huenda zikaanza kunyesha mwishoni mwa mwezi Septemba au mwanzo ni mwa Oktoba, ushauri ukatolewa juu ya suala la utoaji taarifa za haraka iwapo linatokea jambo kwa ajili ya msaada wa haraka ameeleza Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Magu Mohamed Kyando

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI SGR NA KUZINDUA MELI NNE ZA MIZIGO ZIWA TANGANYIKA

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu