Elimisheni, Sheria ifuate baadae
Wastani wa mifuko ya plastic trilioni moja inatumika kila mwaka duniani, ambapo takribani mifuko milioni 2 inatumika kwa kila dakika. Hata hivyo matumizi ya mifuko ya plastic yanatofuatiana kutoka nchi moja hadi nyingine na Tanzania ikiwemo inakadiliwa matumizi ya mtu mmoja kwa mwaka ni jumla ya mifuko ya plastic 96
Mifuko ya plastic inatokana na rasilimali za gesi asilia pamoja na petrol, ambapo inaweza kudumu katika mazingira ya vipande vipande kwa miaka zaidi ya 100 bila kuteketea na hata ikiteketezwa kwa moto usababisha hewa ya ukaa ambayo ni hatari kwa afya na ikifukiwa ardhini haiozi na kuzuia maji na hewa kuingia ardhini
Mohamedi Semdoe ni Afisa usafi na mazingira wilaya kibondo mkoani Kigoma wakati wa kampeni ya usafi amefafanua kuwa ni vema jamii ikaelimishwa juu mambo mbalimbali ambayo serika inakuwa imeamua yafanyike likiwemo la usafi badala ya kukazia sheria zaidi kama alivyoamua kutengeneza Godoro lililotokana na mifuko ya Plastic ambapo jamii itahamasika katika swala la usafi wa mazingira bila kutumia sheria kali na kisha kuleta tija
.
Amefafanua kuwa kulingana hali ilivyo mifuko hiyo haizuiliki na hakuna njia mbadala hali inayoendelea kusababisha mifuko ya Plastic kuzagaa mijini na Vijijini na inaweza kutumiwa na jamii lakini kama elimu itatolewa kwani mifuko hiyo inakusanywa majalalani na kusafishwa na kutengeneza godoro
Baadhi ya wananchi waliopata maelekezo ya usafi na mazingira kwa kutengeneza magodoro yanayotokana na Mifuko ya plastic wameeleza kuwa ni vema elimu hiyo ifike vijijini ambako ndiko iliko jamii kubwa yenye maisha ya kiwango cha chini nambayo ndo yenye kutmia magodoro hayo kuliko watu walioko mjini
Katika swala la kutoa ajira Baraka Ramadhani anasema kuwa yeye kama fundi nguo, amepata kazi kutengeza kava za kwa ajili ya kuweka mifuko midogomidogo tayari kwa kutumia kwenye vitanda huku watu wanaopewa kazi ya kukusanya mifuko malalani ulipwa shilingi mia 1 kwa kila mfuko.
Hata hivyo wakazi wa kibondo pamoja na kupongeza ubunifu huo wasema nilazima hatua za afya ziangaliwe kwasababu mifuko hiyo walio wengi wanaikusanya majalalani ili kuepuka magonjwa ya milipuko yanayotokana na uchafu, huku Jonstoni Masunzu mkazi wa kijiji cha Kumsenga akisema kulingana na hali ngumu ya maisha ya kijijini wao utumia mikeka kulalia uenda Magodoro yakaleta unafuu
Kwa upande wake Ayubu Sebabili Katibu Tawala wilaya ya Kibondo katika anazungumza kuwa katika swala la kudhibiti usafi wa mazingira mojawapo ni sheria lakini kikubwa ni elimu katika jamii kuliko kutumia sheria na nguvu
Kumekuwepo na utaratibu wa kuzuia mifuko ya plastic katika maeneo mengi hapa nchini huku kukiwa hakuna njia mbadala ya kupata vifungashio hali inayopelekea zoezi hilo kukwama na mifiko hiyo kusambaa kwa wingi
Mwisho
Mohamed Semdoe Afisa usafi na Mazingira wilaya Kibondo |
Baraka Ramadhan Findi cherehan akiandaa kava la Godoro la mifuko ya Plastic |
Mwanaume akiwa jalalani akikusanya mifuko ya Plastic tayari kwa kuiuza kwa watengenezaji wa mifuko ya Plastic |
Kitanda chenye Dodoro lilitengenezwa kwa Mifuko ya Plastic |
Maoni
Chapisha Maoni