Watakiwa kusalimisha Siraha Haramu kwa muda uliopangwa
Watakiwa kusalimisha Siraha Haramu kwa muda uliopangwa
Mrakibu wa Polis Marko Joshua Ocd Kibondo |
Katika hatua ya kuboresha hali ya usalama hapa nchini,Jeshi la Polisi kuanzia june 12 mwaka huu lilitoa muda wa kusalimisha siraha haramu kwa iyali zinazomilikiwa kinyume cha sheria
Mkuu wa Polis wa wilaya kibondo mkoani kigoma Marko Joshua alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana, ameitaka jamii kuutumia vizuri muda uliotolewa na serikali kwa kuhakikisha kila mtu anayemiliki siraha yoyote kinyume cha sheria anaisalimisha ili kudumisha dhana ya kutii wa sheria bila shuluti na kuongeza kuwa mtu anaweza kupeleka katika ofisi ya kata au kijiji au kituo chochote cha polisi na asisumbuliwe
Joshua amesema kuwa muda uliotolewa na serikali ni kuazia june 12 hadi september 12 mwaka huu, kwa yule ambaye hatafuata utaratibu huo, kutapitika msako mkali ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale watakao bainika kwani mpaka sasa hakuna siraha iliyokwisha salimishwa na kuwataka viongozi wa dini kuwaelimisha waumini wao, madhala ya kumiliki siraha haramu
Siraha haramu zinatajwa kutumika katika vitendo vya uharifu kama ujambazi, uwindaji haramu, kwenye mapori ya akiba na hifadhi za Taifa na utekeji wa magari huku, mtendaji wa kijiji cha kagezi Kazala Dama,s akieleza kuwa katika kijiji chake hakuna mtu aliyekwisha salimisha siraha na kuda kudai kwa hivi sasa hali simbaya sana ikilinganishwa na siku zilizopita watu walikuwa wakivamiwa na kunyang’anywa mali zao hasa maeneo ya mipakani
Laurence Kagina ni mkazi wa kijiji cha Kibuye kilichoko mpakani mwa Tanzania na Burundi yeye anasema kuwa baada ya seikali kuweka vituo vya polisi karibu na vijiji vya mpakani na katikati hali imekuwa nzuri maana waarifu wamekuwa wakishirikiana watu kutoka Burundi na kuwavamia watanzania na kuwanyang;anya mali zao na kusababisha hata vifo
Aidha wakazi wa maeneo ya kibondo wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu juu ya umiliki wa siraha haramu kwani hatari sana zinapoendelea kuwemo miongoni mwa jamii kama alivyoeleza Tahabiti Yusuph mkazi wa Kigina huku mchungaji wa kanisa la T.A.G Emmanuel Koreshi akisistiza kutolewa maelekezo kwa makundi tofauti kwani elimu na ujumbe haujaifikia jamii inavyotakiwa maana yeye hajasikia kama kuna iliyosalimishwa
Katika mkoa wa Kigoma kumekuwa kuwa kukiripotiwa vitendo vya uharifu wa kutumia siraha vinavyosadikiwa kuwa vinafanywa na majambazi vijijini huku baadhi ya wananchi wakiwashutumu wakimbizi wanaohifadhiwa hapa nchini kwa kukimbia machafuko katika nchi zao na wengine kutoka katika nchi mojakwamoja na kushirikiana na wenyeji wa Tanzania kwasababu mkoa huo unapakana na nchi za Burundi na Kongo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni