Kugombea pamoja si uadui bali tushikiane ili kuijenga Tanzania ijayo
Wanaotarajiwa kuingia katika kinyang,anyiro cha uchaguzi mkuu hapa nchini kuwani viti
mbalimbali vya ubunge Udiwani na Urais wametakiwa kujenga umoja kwa wananchi
wanaotakiwa kuwapigia kura pasipo kuwagawa
na kusababisha hali ambazo hazistaili katika Taifa
Akiongea kwenye mkutano wa adhara mjini kibondo mkoa wa
kigoma mbunge anemaliza muda wake Felix Mkosamali amsema kuwa kuwa kitendo cha
kugombea au kutafuta nafasi moja mkiwa wengi si uaduai hata kama kuna itikadi
tofauti za vyama bali kila mgombea anatakiwa kutambua kuwa hii nchi ni mali ya
watanzania wote na kinachotakiwa ni kuacha malumbano
Amesema kuwa hali hiyo ya mgawanyiko inayowakumba wengi na
kuamua kuwaingizia wafuasi wao mambo yanayoweza kusababisha vurugu na kuvunja
undugu hatua inayoonyesha taswila ya kutokomaa kwa siasa katika Tanzania
na Bara la Afrika
Mkosamali katika mkutano amejiata kuwa nae mwaka huu
amechukua fom ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Muhambwe kupitia umoja wa
katiba ya wananchi Ukawa kupitia chama cha NCCR Mageuzi
Kutokana na ahli hiyo amewataka wananchi wa Kibondo kufanya
kampeni zenye ustarabu hasa kilenga na kutarajia matokeo mazuri baada ya
uchaguzi na ktika kuliendeleza Taifa maana maana watanzani wengi wanakabiliwa
na changamoto nyingi ambazo zinawapelekea kuhitaji viongozi mahili na wazalendo
Nae Afisa uchaguzi Jimbo la Buyungu Bw, Adam. A. Adam
amefafanua kuwa watanzania wengi hawana elimu ya kuendesha kampeni na namna ya
upigaji kura hali inayowapelekea wengi kujikuta wameingia katika mikono ya
sheria kwa kwenda kinyume na taratibu na kuwataka wagombea wote kuwaelimisha
wafuasi wao kwani wenyewe upewa maelekezo ya kuendesha kampeni
Aidha ameongeza kusema kuwa muda wa vyama vyote kutoa
matangazo ya kampeni nikuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa mbili usiku na
kuelekeza kuwa chama chochote hakitakiwi kutoa matangazo yake kabla na baada ya
muda huo na kuda kuwa wataendelea kuelekezana na viongozi na kuonyana kabla ya
kuchukua hatua za kisheria ila atakaeonyesha kuendelea kukiuka utaratibu hatua
zaidi zitachukuliwa
Felix Mkosamali mbunge anaemaliza muda wake Jimbo la Buyungu |
Maoni
Chapisha Maoni