Ni wazi kuwa maisha katika uso wa Dunia hutegemea huduma ubora wa huduma zitolewazo na mazingira husika. Ukiangalia mfumo wa ikolojia wa misitu, bahari, mbugani na kwenye udongo utaona uwepo wa maji, hewa nzuri na rutuba ya udongo ndivyo vinavyopelekea wanyama na mimea kuwepo na kupendezesha mazingira.


Eneo la Igamba katika Mto Maragalasi ambako waligundulika vyura na Konokono wasiopatikana kokote Duniani ambapo lilitakikiwa kujengwa kituo cha kufua umeme 

Baadhi ya washiriki wa semina ya uhifadhi viumbe hai na Mazingira iliyofanyika Kazulamimba 


Donald Kasongi mkurugenzi mtendaji shirika la Governance Links akiwa mwezeshaji katika semina ya uhifadhi wa mazingira Kazulamimba


Pantaleo Shoki Mkurugenzi wa utafiti na sera shirika la Governance Links

Ni wazi kuwa maisha katika uso wa Dunia hutegemea huduma ubora wa huduma zitolewazo na mazingira husika. Ukiangalia mfumo wa ikolojia wa misitu, bahari, mbugani na kwenye udongo utaona uwepo wa maji, hewa nzuri na rutuba ya udongo ndivyo vinavyopelekea wanyama na mimea kuwepo na kupendezesha mazingira.

Wakazi wa kata ya Kazulamimba wilaya ya uvinza mkoani Kigoma wamepata kujifunza kuhusu uhusiano uliopo kati ya mazingira na maisha ya viumbe hai katika uso wa Dunia. Waliweza kutambua kuwa Mazingira  ni jumla ya mambo yote yanayotuzunguka ikijumuisha viumbe hai na vile visivyo hai. Viumbe hai ni pamoja na binadamu, wanyama na mimea na vile visivyo hai ni pamoja na hewa, Jua, udongo hivyo shuguli za maendeleo hazitakiwi kuathili mazingira yetu

Donald Kasongi ni mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Governace Link  linalilojihusisha na utunzaji wa mazingira na viumbe hai lenye makao makuu yake Jijini mwanza, katika semina elekezi ilyofanyika Katika kijiji cha Kazulamimba amesema kuwa wananchi hawanabudi kufahamu umuhimu wa kutunza mazingira  na viumbe hai hasa wananchi wanaoishi kwa kuzunguka Bonde la Mto Maragalasi ambako kuligundulka vyura na Konokono ambao hawapatikani kokote Duniani


Aidha amesema kuwa katika mto Maragalasi kulikotakiwa kujengwa mitambo ya kufua Umeme baada ya kuonekana kuwa eneo hilo lina viumbe hai hao, wanaojulikana Kama Igamba Snail na Goby Chichlid,  Bank ya Dunia iliamua kujitoa katika ufadhili wa mradio huo ili viumbe hao wasije wakatoweka hasa kwa faida ya Vizazi vijavyo na kwakuwa Tanzania ilisaini mkataba wa Kimataifa wa kulinda Rasilimali na viumbe hai iligaili kuendeleza ujenzi huo


Kauli hiyo ilipingwa na baadhi ya washiriki wa kikao hicho wakidai kuwa kama ni kwa vizazi vijavyo vitauliza kuwa kwanini kulikuwepo na Mto huo na haukutumika katika shuguli mbalimbali kama za kilimo cha umwagiliaji badala yake wazazi wao walibaki masikini ambapo mmoja wa washiriki Emmanuel Kimpante ambae alitaka shuguli za ujenzi wa mitambo nazi zingine za kijamii ziendelee katika Bonde hilo la Mto Maragalasi


Pantaleo Shoki  ambaye ni Mkurugenzi wa utafiti na Sera wa shirika hilo ye alisema kuwa ni kweli kazi za maendeleo katika jamii zinatakiwa kufanyika ila zihatili na kuleta uharibifu mkubwa wa mazingira na kuongeza kuwa hivi sasa katika mto huo kuna shuguli nyingi zinaendelea kama kuchoma mkaa, kilimo na kuchimba chokaa bila utaratibu maalum za kinga ya uhifadhi wa   Mazingira


Hata hivyo waliongeza kuwa serikali imekuwa ikipiga marufuku kufanya shuguli mbalimbali katika Mto huo huku maeneo yake hayalindwi hata kidogo mambo yanayofanyika ni kama kiini macho hali inayozidi kuzua malamamiko katika jamii


Nao Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamsema kuwa kinachochanganya ni serikali na Taasisi mbalimbali kutowashirikisha wakazi wa maeneo husika mara inapotakiwa kujenga mradi wa maendeleo kwa kuwaleza faida hathali zinazoweza kujitokeza  ili wajue kutafuta kinga za uharibifu wa mazingira huku Afisa maliasili wa wilaya hiyo Bw Wejo Juma Wejo  akisema kuna mambo wanayoshirikishwa wananchi lakini kuna changamoto kutoka serikali kuu ya kutoishirikisha halmashauri kwa kuleta wachimbaji madini bila taarifa


Semina hiyo elekezi iliwahusisha viongozi wa Asasi mbalimbali Tanesco na Baadhi ya Wakuu wa Idara za halmashauri ya wilaya uvinza na kufafanyika kwenye Wilaya zinazonguka Mto huo ambazo ni Kibondo Kakonko Buhigwe na Kasulu na kutakiwa kuhakikisha utanzaji wa mazingira unataliwa mkazo


Mwisho   

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji