Mahakama ya Wilaya ya kibondo mkoani Kigoma imemuhukumu Mkazi mmoja wa kijiji cha Muhange Wilaya Kakonko kutumikia adhabu ya miaka 7 gerezani au kulipa faini ya shiringi milioni 6 baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha watoto wa wili raia wa kigeni kutoka nchini Burundi.

Mahakama ya Wilaya ya kibondo mkoani Kigoma imemuhukumu Mkazi mmoja wa kijiji cha Muhange Wilaya Kakonko  kutumikia adhabu ya miaka 7 gerezani au kulipa faini ya shiringi milioni 6 baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha watoto wa wili raia wa kigeni kutoka nchini Burundi.

Mbele ya hakimu Mkaazi  wa Mahakama ya wilaya ya kibondo Bw.  Mlokozi Mkamuntu Mwendesha mashitaka wa Idara ya Uhamiaji  Bw. Baraka Manga   amemtaja mtuhumiwa  huyo kuwa ni  Norbeth Dominico mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa kijiji cha Muhange Wilayani Kakonko.

Mwendesha mashitaka wa idara ya uhamiaji Bw.Manga amesema kuwa mnamo Augost 16 mwaka huu, majira ya saa 11:00 asubuhi katika kituo cha Polisi cha ukaguzi wa magari mjini Kakonko mtuhumiwa alikutwa na watoto wa kike wa wili akiwasafirisha kutoka nchini Burundi kuelekea Mkoani Shinyanga kinyume na sheria.

Aidha katika maelezo ya awali Bw. Manga amewataja watoto hao kuwa ni Miuelle Emmanuel mwenye umri wa miaka 16 na Safina Adamu mwenye umri wa miaka 17 wote wakiwa na raia wa nchi jirani ya Burundi ambao wamerudishwa nchini kwao.

Hata hivyo mahakama imetoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa watu wenyetabia ya kusafirisha watoto na mtuhumiwa ameshindwa kulipa faini hivyo anatumikia adhabu gerezani.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji