Vijana hapa nchi wametakiwa kujitambua kuwa wao ni kundi muhimu sana na linalotegemewa kama nguvu kazi ya Taifa, hivyo kutokana na hali hiyo wasikubali kutumiwa vibaya katika jambo lilote hasa katika kipindi hiki cha kampen za kuelekea uchaguzi mkuu oktoba 25 mwaka huu
Vijana wametakiwa kujitambua
Vijana hapa nchi
wametakiwa kujitambua kuwa wao ni kundi
muhimu sana na linalotegemewa kama nguvu
kazi ya Taifa, hivyo kutokana na hali hiyo wasikubali kutumiwa vibaya katika
jambo lilote hasa katika kipindi hiki cha kampen za kuelekea uchaguzi mkuu
oktoba 25 mwaka huu
Akiongea kwenye mkutanu wa uzinduzi wa kampeni za chama cha mapinduzi uliofanyika
katika Tarafa ya kifura wilaya kibondo mkoani Kigoma, aliyekuwa mgombea Ubunge
kura za maoni kisha kuengeliwa na halmashauri kuu ya Ccm, Jamal Abdalah amesema
kuwa vijana wengi hawajaweza kujitambu umuhimu walionao hali inayopelekea
kurubuniwa na kujiingiza katika vitendo visivyostaili
Jamal aliyekuwa mshindi katika kura za maoni na kuondolewa
katika nafasi hiyo, amezidi kumnadi mgombea aliyepata nafasi ya tatu na baadae kuteuliwa kuwa mgombea ubunge jimbo
la Muhambwe Atashasta Nditiye amewataka wanachama wa ccm na vyama vingine hususa vijana kutokubali
kutumiwa vibaya katika uchaguzi 2015 na kuacha makundi wao wafanye maamuzi mema
Uzinduzi wa kampeni hizo ccm zilitaka kuingiwa na dosari
baada ya baadhi vijana ambao
hawakufahamika majina yao kwa haraka kutajwa kuwa walitaka kuleta vurugu na
kuanza kurushiana maneno na katibu wa chama hicho Bw, Hamis Kananda na baadae
gasia hizo kuzimwa
Kampeni hizo zilizozinduliwa jana kote nchini, kwa upande wa
jimbo la Muhambwe umoja wa katiba ya
wananchi ukawa waliendesha mkutano wao katika kata ya Kibondo mjini, ACT Wazalendo haijafahamika watazindua lini,
kwa kumnadi mgombea wao Bw Edgar Mkosamali wakati Chama cha Chauma kimeandaa
kuzindua kampeni zao jumatano wiki hii kikiwakilishwa na Nduilabusa mapigano, huku wagombea ubunge wa Ccm na Ukawa kupitia
NCCR Mageuzi ambao ni Atashasta Nditiye na Felix Mkosamali wakijinadi kwa ahadi
mbalimbali
Kampeni hizo ilizoanza jana Agast 22 ni kwa ajili ya
kuwanadi wagaombea urais, Ubunge na
Udiwani kwa vyama vyote vya siasa hapa nchi kuelekea uchaguzi mkuu ambapo
watanzania wote wanatakiwa kuwa watulivu waadilifu na kuchukua maamuzi yenye
tija kwa ajili ya uendelevu wa taifa lao bila kufuata ushabiki wotewote kwa
kukumbuka kuilinda Amani ya nchi hii kwani imo mikononi mwao wenyewe
Wananchi wakimsikiliza mgombea ubunge mjini kibondo |
Add caption |
Wananchi na wanachama wa ccm wakiwa kwenye kampen za uchaguzi |
Jamal Abdalah aliyeengeliwa na NEC akimnadi mwenzake katika mkutano wa kampeni |
Atashasta Nditiye mgombea ubunge jimbo la Muhambwe 2015 |
Maoni
Chapisha Maoni