Mkuu wa jeshi la polisi wilayani kakonko mkoani kigoma Bw. Filimoni Makungu amewataka wanasiasa kutumia sera zao kuwashawishi wananchi katika kampeni zao na kuepuka lugha za uchochezi ambazo huweza kuleta vurugu baina yao.

Mkuu wa jeshi la polisi wilayani kakonko mkoani kigoma Bw. Filimoni Makungu amewataka wanasiasa kutumia sera zao kuwashawishi wananchi katika kampeni zao na kuepuka lugha za uchochezi ambazo huweza kuleta vurugu baina yao.

Filmon Makungu Ocd Kakonko
Wito huo  ameutoa wakati akizungumza na na clouds  ofsini kwake alipo kuwa  akizungumzia mchakato wa jeshi la polisi wilayani humo walivyo jipanga katika kudhibiti vitendo vya uvunjifu wa amani hasa wakati wa kampeni mbalimbali za uchaguzi mkuu.

Bw.Makungu amesema tume ya uchaguzi imetoa maelekezo mazuri kwa wagombea na hivyo hatarajii kuona kampeni za uchochezi na lugha chafu na kwa wale amabao  wataenda kinyume na maelekezo ya tume ya uchaguzi sheria zitachukua mkondo wake.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halimashauli ya wilaya ya kakonko Bi.Jaina Msangi amesema wagombea kutoka vyama mbalimbali wanapokuja kuchukua fomu wamepewa maelekezo ya kutosha na hivyo hatarajii kuona dosari kwa wagombea hao wakati wa  kampeni zao

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji